Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,308
- 18,485
Kesi ya uhaini Na. 19605/2025 inayomkabili Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Taifa Tundu Lissu inaendelea tena leo, Alhamisi Februari 12.2026 kama ilivyo ada mbele ya jopo la Majaji watatu (3) wakiongozwa na Jaji Dastan Ndunguru.
Jana (Jumatano, Februari 11.2026), Mahakama ilitoa uamuzi mdogo wa mapingamizi matano (5) yaliyokuwa yamewekwa na mshtakiwa Tundu Lissu ambaye anajitetea mwenyewe kwenye kesi hiyo, ambapo manne (4) kati ya mapingamizi hayo yalitupiliwa mbali huku moja (1) likikubaliwa.
Moja lililokubaliwa na Mahakama ni lile linalohusu kizimba maalum kilichojengwa kwenye chumba cha Mahakama kwaajili ya kutumiwa na mashahidi wa siri (raia), ambapo Mahakama iliagiza kizimba hicho kifanyiwe marekebisho ili Majaji waweze kumuona shahidi, sambamba na kufuatilia mwenendo wako akiwa kwenye kizimbani.
Soma > Kesi ya Lissu: Mahakama yaagiza Kizimba cha Mashahidi wa siri kirekebishwe Majaji wawaone. Kesi kuendelea Feb 12, 2026
Hata hivyo, Mahakama ilitoa uwanja kwa upande wa Jamhuri, kwamba endapo marekebisho ya kizimba hicho yatakuwa yamekamilika basi wanaweza kumleta shahidi wa siri kama walivyokusudia awali (kwamba shahidi wa 4 wa Jamhuri ni wa siri), na endapo marekebisho hayo yatakuwa hayajakamilika basi upande wa Jamhuri unaweza kuleta shahidi asiyekuwa wa siri (Askari) ili atoe ushahidi wake Mahakamani,
Maagizo ya Mahakama yalienda mbali zaidi kwa kueleza kuwa, endapo chumba namba moja (1) cha Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo ya Dar es Salaam kinachotumika kusikilizia kesi hiyo kitakuwa bado kwenye 'matengenezo (marekebisho ya kizimba)' kesi hiyo haitasimama kwani kitatumika chumba kingine, miongoni mwa vyumba vilivyopo Mahakamani hapo.
Hivi ndivyo Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu, alivyofikishwa Mahakama Kuu asubuhi ya leo kwa ajili ya kuendelea na usikilizwaji wa kesi inayomkabili. Inatarajiwa kuwa shahidi wa siri, anayedaiwa kuwa askari, atapanda kizimbani na kutoa ushahidi wake katika shauri hilo.
Lissu amewasili Mahakamani hapo chini ya ulinzi, huku akipokelewa na wafuasi, viongozi wa chama chake pamoja na wananchi waliokusanyika kufuatilia mwenendo wa kesi hiyo yenye mvuto mkubwa wa kisiasa na kijamii.
Kesi hiyo inaendelea kusikilizwa katika Mahakama Kuu huku upande wa utetezi na mashtaka ukiendelea kuwasilisha hoja zao mbele ya mahakama.
Mashahidi wa upande wa mashtaka wameanza kutoa ushahidi dhidi ya Tundu Lissu, kiongozi wa chama kikuu cha upinzani Tanzania, CHADEMA ambaye anayekabiliwa na kesi ya uhaini katika mahakama kuu jijini Dar esSalaam.
Sehemu ya 160; Kesi ya Uhaini ya Lissu
Ni siku nyingine, karibuni tena leo kwenye mwendelezo wa kesi.
Mhe. Lissu tayari ameingia, kama kawaida Wananchi wamepiga shangwe ile ya Rais! Rais! Rais!
Majaji nao wameingia kama kawaida yao wapo watatu.
Naona Kizimba kimetobolewa kidogo upande wanaokaa Majaji ila kama shaidi ni mfupi hata Majaji hawawezi kumuona ila tuendelee.
Jaji Ndunguru anasema sasa tuendeleee.
Anasimama Wakili wa Serikali Renatus Mkude Wakili wa serikali Mkuu anasaidiwa na Ajuaye, Katuga, Ignas, Thawabu, Cathbert na Winiwa Kasawa tunaiwakilisha Jamhuri na mshitakiwa yupo hapa Mahakamani.
Shahidi P11 ana dharula lakini leo tumekuja na P5 leo kama atakuwa tayari tutaendelea.
Jaji Ndunguru anasema Mshitakiwa unasemaje?
Mh. Lissu anajibu anasema kimsingi niko tayari isipokuwa niliambiwa ni P11 sasa nipeni dakika 5 niyatafute maelezo ya huyo P5 niyapate kwanza hapa halafu tuendelee kushughulika nae mimi sina shida kabisa.
Ngoja nitafute hayo maelezo yake vizuri.
Jaji Ndunguru anasema sasa sisi tunakupa dakika 10 sio tatu na unaruhusiwa kukaa pia sio lazima usimame sana hapo.
Lissu anajibu hakuna shida kabisa Waheshimiwa Majaji.
Mheshimiwa Lissu ametafuta kidogo makabrasha yake hapa amepata hayo maelezo amekaa kuyasoma na amemaliza anasema tunaweza kuendelea Waheshimiwa majaji.
Jaji Ndunguru tunamuomba shahidi.
Anasimama Renatus anasema shahidi ataongozwa na Wakili Ajuaye Nzengeli Wakili wa Serikali.
Anasimama karani anateta jambo na Jaji anashuka chini kuongea na Mawakili wa Serikali.
Anarekebisha mitambo pale.
Tunasubiri kuona nini kinaendelea.
Anaingia askari mmoja kwenye kile kizimba, anapelekewa kipaza sauti huyo shahidi.
Kile kizimba kimefunguliwa kidizaini ambayo Majaji wao wanadai wanamuona.
Jaji anasema tutamuuliza kuhusu umri wake na dini yake kabla ya kutoa ushahidi wake.
Umri wangu ni miaka 33.
Dini yangu ni Muislamu.
Huyo ni Shahidi P5 Ambae ni shahidi wa nne (4) kwa maana ya (PW 4) lakini jina lake alilobatizwa ni P4.
Ajuaye anasimama anasema shahidi unanisikia hapo?
Unaishi Wapi?
Naishi Kibangu, Ubungo Mkoa wa Dar es salaam.
Anasema anafanya kazi ya Machinga, mjasiriamali, saa nyingine naosha magari.
Unauza bidhaa gani?
Nauza viatu, saa zingine nauza soksi.
Shughuli zangu nafanyia Mchikichini, Kariakoo, Posta ya zamani, Feri hadi Posta Mpya.
Ajuaye anaendelea kumuhoji hapa na shahidi anajibu kama ninavyowaeleza.
Elezea sasa bidhaa zako unachukulia wapi?
Shahidi wa kificho ; Ilala Boma, Sokoni..
Eleza tarehe 04/04/2025 ulikuwa wapi?
Shahidi wa Kificho: Nilikuwa Posta ya zamani Garden eneo la NBC Bank nikiwa naperuzi mitandao ya kijamii kwenye simu yangu?
Ajuaye: Sasa eleza ulikuwa unaperuzi kwenye mtandao gani?
P5: Facebook, WhatsApp na Youtube, nilikuwa naperuzi kwa kutumia simu yangu aina ya smartphone sonny experior Galaxy
Sasa wataalamu wa simu mtatusaidia hapo hiyo aina ya sim sie wengine hatufahamu zaidi. Acha tuendelee kumsikiliza shahidi.
Anaendelea hapa.
Wakati naperuzi niliona video ndogo ikimuonesha Tundu Lissu, niliona video Facebook.
Ni kama Majaji wamechoka wanamshangaa Shahidi, sisi hatumuoni lakini sura za majaji ni kama wanakunja.
Niliingia faceebok kwanza lazima uwe na account na bando la kutosha. Mimi niliingia kwasababu nilikuwa tayari nina account yangu.
Maswali anayoulizwa shahidi na Wakili wa Serikali na Majibu yake ni kama anajibu kwa kusoma mahali maana kuna muda anajibu jibu ambalo haliendani na swali.
Video ilikuwa ya Tundu Lissu, mimi namfahamu kwa kutumia vyombo vya habari na mitandaoni.
Wakili wa Serikali : Na wewe binafsi unamfahamuje?
P5 : Na mimi namfahamu.
Basi nikubadilishie swali, Tundu Lissu ni nani?
Shahidi: Tundu Lissu ni mwanasiasa.
Sehemu ya 161
Anaendelea Wakili wa Serikali
Ajuaye: Ulipoona video ulifanya nini?
Shahidi: Nilifungua na kucheza kutaka kuona anasema nini?
Nikacheza na kumsikia akisema atahakikisha uchaguzi wa 2025 haufanyiki ataenda kukinukisha.
Hiyo ameisema kwa kutamka neno moja moja.
Majaji wanasema rudia.
A ta ha ki ki sha u chagu zi A TA KI NU KI SHAAA.
Uchaguzi ulikuwa unahusu madiwani wabunge na Rais.
Ajuaye anaendelea kumuhoji.
Kingine alisema Polisi wanatumika kuiba kura, pia nilisikia akisema Majaji nao ni MaCCM hawatendi haki Mahakamani.
Video hiyo ya Tundu Lissu niliona akiwa amesimama Jukwaani.
Niliona pia Tundu Lissu amevaa gwanda za kaki na tisheti nyeusi ndani akiwa amevalia miwani na bendera ya taifa kwa nyuma.
Ajuaye: Elezea sasa baada ya kuona video hiyo ulifanya nini?
Mimi nilivyoona nikaendelea kuperuzi mitandao na kupumzika kuelekea kituo cha daladala na kurudi nyumbani ubungo.
Baada ya kushuka kituo cha daladala nikawa naelekea maskani kijiwe cha kahawa.
Jaji anasema wapi huko?
Shahidi anaguna. Hiyo maskani ametaja kama ni eneo linaitwa hivyo, ameulizwa tena ni kama amechanganyikiwa.
Nilipofika kituo cha kahawa nilikuta mzozo wa video vya Tundu Lissu na kila mmoja alikuwa na hoja zake.
Wengi walikuwa wanamuunga mkono kukinukisha na walisema siku ya uchaguzi hawataenda kupiga kura.
Baada ya hapo mimi nikaona siku ya Uchaguzi kutakuwa na fujo kubwa.
Pia niliona kupitia mzozo huo amani itavunjika na sisi wafanya biashara tutashindwa kupata kipato na tutapata njaaa.
Watu wanacheka hapa.
Baada ya hapo nilitoka kwa kwenda nyumbani na kumpigia ndugu yangu Rama haya maswala kupitia Tundu Lissu.
Jamaa linasoma huko kizimban hata kusoma halijui. Sijui sasa pale majaji wanamuangalia nini na pia hata aliyemuandikia cha kusoma nae ni kilaza. Ngoja tusubiri.
Huyo ndugu yangu anafanya kazi ni Polisi, Askari Polisi.
Huyo ni Polisi wapi?
Ni Polisi Relini Tabata, sio ni Tabata relini.
Huyo ndugu yangu alinijibu kuwa tumesikia tunalifanyia kazi kikamilifu.
Daah! huyu shahidi alikuwa na ndugu ambae ni Polisi amempigia simu siku hiyo hiyo akawa anajua kuwa hilo suala linafanyiwa kazi huyu kwenye cross atapasuka sana.
Tarehe 04/09/2025 nilienda Central Polisi baada ya kupigiwa simu na kwenda kutoa maelezo.
Pale Polisi Central alinichukua askari na kwenda kunichukua maelezo kupitia ile video ya Polisi.
Mlikutana vipi na huyo Polisi?
Alikuwa ananihoji. Ndio jibu lake.
Ajuaye anaendelea.
Nilivyofika pale niliipigia ile namba iliyonipigia.
Alinifuata na kunichukua na kunipeleka ofisini kwenda kuhojiwa kuhusu ile video ya Tundu Lissu.
Baada ya kumaliza mahojiano na Polisi nilitoka na kwenda nyumbani.
Una kingine?
Kile kilichonitilia hofu na uoga ni ile kauli ya kukinukisha, nilikaaa siku sita kipindi cha uchaguzi na njaa ilinipiga kweli kweli.
Ajuaye anasema Waheshimiwa Majaji kwa shahidi huyu ni hayo tu.
Watu wanaangaliana tu na kutabasamu na kucheka.
Shahidi amemaliza. Tunasubiri aulizwe maswali hapa.
Majaji wanaandika hapa na Mheshimiwa Lissu ameng'ata kalamu yake anasoma makaratasi kadhaa.
Majaji wamemaliza.
Wanasema maswali ya Dodoso?
Anasimama Mhe. Lissu.
Huu ndio ushahidi umeniweka Gerezani miezi 10?
Jaji: Naomba tuendeleee na Maswali.
Lissu: shahidi unanisikia?
Shahidi wa kificho: Nakusikia.
Lissu: Umesema unafanya kazi ya umachinga?
Shahidi wa kificho: Kweli nafanya.
Sehemu ya 162
Anaendelea Mhe. Lissu na maswali ya Dodoso
Lissu: Una leseni ya biashara?
Shahidi wa Kificho; Leseni ya Biashara sina ila ninayo naiandaaa.
Lissu: Una kitambulisho cha NIda?
Shahidi wa kificho; Sina ila napambana nikipate.
Lissu: Una kitu chochote cha kukutambulisha ni mfanyabiashara zaidi ya maneno yako?
Shahidi wa kificho: Kile ninachotembeza ndio ushahidi wangu.
Lissu: Umekileta hapa?
Shahidi wa kificho; Sijaleta.
Lissu: Watajuaje we ni mfanyabiashara.
Shahidi wa kificho: Waniamini tu.
Lissu: Unakaa ubungo kibangu?
Shahidi wa kificho: Ndio.
Lissu: Umeleta mkataba wa pango? Au umesema unakaa nyumba gani?
Shahidi wa kificho: Sijaleta ila labda niende nao Ubungo Kibangu wakapaone.
Lissu: Unadhani majaji hawana kazi hadi waende kibangu?
Shahidi wa kificho: Sijui wao.
Lissu: Unakumbuka ulitoa maelezo kule Polisi?
Shahidi wa kificho: Ndio nakumbuka.
Lissu: Waheshimiwa naomba apewe maelezo yake huyu P5 ayaone.
Wanamtafutia. Wameyapata. Wamempa huko kwenye kiboksi chake.
Shahidi wa kificho: Haya ndio maelezo yangu niliyoandika Central Polisi.
Lissu: yana sahihi yako
Shahidi wa kificho: Ndio yana sahihi yangu.
Lissu: Mhe. Nataka nimsomee shahidi maelezo yake anamsomea hapa maelezo yake yote.
Anasema anajishughulisha na kuuza maeneo mbalimbali posta na kuosha magari.
Niliona video ya Tundu Lissu ambae ni Mwenyekiti wa Chadema aliyesema mwaka huu hakutakuwa na uchaguzi na nitakinukisha.
Baada ya kumaliza mizunguko yangu nilirudi Ubungo Riverside na nilipita kijiwe cha kahawa yupo rafiki akaonesha video ndefu sana tofauti na ile niliyoiona mimi. Wengine walimuunga mkono Lissu wengine walipinga.
Baada ya kuona video nikaona nchi inaenda kuingia kwenye vurugu na itatuathiri sisi tunaotafuta riziki mitaani.
Nikamtafuta ndugu yangu ambae ni Polisi kuhusu maneno ya Tundu Lissu na akanijibu tumeyasikia na tumeyaona.
Nikapigiwa simu na Polisi na kwenda Central kutoa ushahidi.
Lissu anasema sasa nataka kukuhoji kuhusu.
1. Mambo ya aina ya simu yako sijaona kwenye maelezo yako.
2. Namfahamu Lissu kutokana na vyombo vya habari. Hayapo kwenye maelezo.
3. Maskani kijiwe cha kahawa hayapo kwenye maelezo.
4. Mtu uliyempigia simu anafanyakazi Tabata Relini. Hayapo pia
5. Ulipata hofu hayo pia kwenye maelezo yako kulikuwa na hofu.
6. Ulipofika Central ulimpigia simu huyo askari hayapo kwenye maelezo.
7. kwamba ulipigwa na njaa kwelikweli siku 6 ulizokaa
Tundu Lissu anaendelea kusoma amesoma maeneo zaidi ya 14 anayotaka kumkanusha shahidi ameyasema Mahakamani lakini kwenye maelezo yake ya Polisi hakuna.
Lissu: Je ungependa maelezo yako haya yawe sehemu ya ushahidi hapa Mahakamani.
Shahidi wa kificho: Sijakuelewa hapo.
Lissu: Je, Ungependa maelezo yako yawe ushahidi Mahakamani?
Shahidi wa kificho: Ndiyo.
Majaji wanateta pale juu.
Mawakili wa Serikali wanaulizwa mnasemaje?
Anajibu Renatus Mkude; Sisi hatuna Objection yanaweza kupokelewa tu.
Majaji wanaandika pale.
Basi maelezo ya P5 yatakuwa ni Kielelezo D3 yaani kielelezo No. 03 cha upande wa Mshitakiwa. Kwa kifupi Mh. Lissu ameshakuwa na vielelezo vitatu upande wake kabla hajaanza kujitetea upande wake. Hadi muda huu Jamhuri hawana kielelezo hata kimoja kilichopokelewa na Mahakama maana vyote vilikataliwa.
Lissu: Waheshimiwa naomba apatiwe maelezo yake.
Shahidi wa kificho: Anapatiwa maelezo yake.
Lissu: Sasa tueleze ulisema unapatia bidhaa zako Ilala boma sokoni sasa angalia maelezo yako na useme hayo maelezo kama yapo?
Shahidi wa kificho: Yapo.
Lissu: Hebu nionyeshe.
Shahidi wa kificho: Amekaa kimya huko anapatafuta.
Lissu: Waonyeshe Majaji mimi siruhusiwi kukuona.
Shahidi wa kificho: Yuko kimya huko.
Lissu: Hayo maneno yapo au hayapo Kaka, natumaini we ni mwanaume.
Sehemu ya 163
Shahidi wa kificho: Hapa hayapo ili nilihojiwa.
Lissu: Safi ukisema hayapo unaokoa muda, sasa uliulizwa kuhusu ulikuwa unafanya nini Posta ya zamani Garden na ukasema ulikuwa unaperuzi Facebook, Whatsapp na YouTube.
Sasa waeleze majaji kama hayo maneno yapo kwenye maelezo yako uliyonayo mkononi?
Shahidi wa kificho: Whatsapp na YouTube hakuna hayajaandikwa hapa na Faceebok na YouTube hapa hayajaandikwa ila nilisema.
Lissu: uliulizwa kuhsuu simu yako na ukasema ni smartphone sony experior galax unakumbuka ulisema hivyo?
Shahidi wa kificho: Nakumbuka.
Lissu: Je, hayo nayo yapo kwenye maelezo yako Polisi?
Shahidi wa kificho: Yapo.
Lissu: Yako wapi? Mstari wa ngapi yapo?
Shahidi wa kificho: Mstari wa tano.
Lissu: Haya soma tuone na mimi nakufuatilia.
Lissu: Hata kama upo kwenye kiboksi utasema tu. Hayapo tukubaliane?
Shahidi wa kificho: Ila Kweli hayapo.
Lissu: Naomba unijibu kama nakosea. Katika maelezo yako yote. Hakuna mahali kokote uliposema ulikuwa na simu kweli au si kweli?
Shahidi wa kificho: Nilikuwa na simu.
Lissu: Nakuuliza kwenye maelezo yako sasa imeelezwa wapi?
Shahidi wa kificho: Hakuna humu.
Lissu: Niko Gerezani miezi 10 kwa ushahidi wa aina hii. Umesema simu yako ulikuwa na account ya Facebook. Shahidi wa kificho: Ni kweli.
Lissu: Kwenye maelezo yako: yako wapi hayo maelezo? Kwamba wewe ulikuwa na account ya Facebook?
Anasimama Ajuaye anasema Mheshimiwa naomba mshitakiwa asitoe matusi kwa shahidi.
Lissu: Sijamtukana nimemuuliza ana akili timamu au hana.
Majaji: Tuendelee hakuna shida.
Lissu: Ulisema ulikuwa na bando la kutosha. Onyesha kwenye maelezo.
Shahidi wa kificho: Yapo hayo maneno.
Lissu: nauliza kwenye maelezo yako Polisi yapo?
Shahidi wa kificho: Yapo nafikiri.
Jaji: Shahidi unatuchanganya. Unaulizwa kuhusu hayo maelezo uliyonayo hapo. Useme kama yapo au hayapo.
Lissu: Ulipoulizwa juu yangu ulisema kwamba unamfahamu Tundu Lissu kupitia vyombo vya habari na mitandaoni na mwanasiasa.
Shahidi wa kificho: Kweli.
Lissu: Onyesha kwenye maelezo yako hayo yako wapi maneno hayi.
Shahidi wa kificho: Hapa hayapo.
Lissu: Ulisema Tundu Lissu alikuwa amesimama Jukwaani.
Shahidi wa kificho: Kweli.
Lissu: yapo kwenye maelezo yako Polisi?
Shahidi wa kificho: Hapa Hayapo.
Lissu: Umesema ulimuona akiwa amevaa magwanda ya kaki, tsheti nyeusi na bendera ya taifa?
Shahidi wa kificho: Ni kweli.
Lissu: Hayo nayo yako wapi kwenye maelezo yako Polisi?
Shahidi wa kificho: Hawa mapolisi hawakuandika na hayo sijui kwanini.
Lissu: Ulisema ulipanda daladala kwenda ubungo na kwenda kijiwe cha kahawa cha maskani?
Shahidi wa kificho: Ni kweli.
Lissu: Je, kwenye maelezo yako polisi na kwenda kijiwe cha Kahawa maskani? Hayo maneno yapo kwenye maelezo yako?
Shahidi wa kificho: Ameunguruma hasikiki.
Lissu: unasema?
Shahidi wa kificho: Kwa hapa sijaona.
Lissu: Ulipofika kwenye kijiwe cha kahawa ulikuta mzozo juu ya video ya Tundu Lissu:
Shahidi wa kificho: Kweli
Lissu: Yako wapi hayo nayo kwenye maelezo Polisi?
Shahidi wa kificho: Hapa haipo.
Sehemu ya 164
Lissu: Uliporudi nyumbani kwako umesema kwamba ulimpigia ndugu yako askari?
Shahidi wa kificho: Kweli.
Lissu: Ulisema anafanya kazi tabata relini?
Shahidi wa kificho: Kweli.
Lissu: Tuoneshe yako wapi kwenye maelezo yako?
Shahidi wa kificho: Hapa hayapo.
Lissu: Huyo ndugu yako askari Polisi ana jina?
Shahidi wa kificho: Ndio jina analo.
Lissu: Polisi umemtaja jina? Waeleze majaji kama kuna mahali umemtaja jina?
Shahidi wa kificho: Sijamtaja.
Lissu: Ana cheo chochote?
Shahidi wa kificho: Sijui kama ana cheo chochote.
Lissu: Ana force no?
Shahidi wa kificho: Sijui hata maana yake mimi.
Lissu: Ulipoangalia ile video ukaona maneno ukapata hofu?
Shahidi wa kificho: Kweli.
Lissu: kwenye maelezo yako wapi?
Shahidi wa kificho: Hapa hayapo hayo.
Lissu: Tarehe 09 siku unaandika maelezo yako Polisi ulipofika Central ulimpigia simu aliyekupigia mwanzoni?
Shahidi wa kificho: Ndio.
Lissu: Uliandika wapi kwenye maelezo yako polisi?
Shahidi wa kificho: Yapo yameandikwa lakini hapa hayapo.
Lissu: Maana yake nini sikuelewi?
Shahidi wa kificho: Hapa hayapo.
Lissu: Yale maneno kwamba tutakinukisha ndio yaliyotokea siku ya Uchaguzi ulisema hivyo?
Shahidi wa kificho: Ndio nimesema.
Lissu: Je, Uliandika maelezo ya ziada polisi ili kujumuisha kilichotokea tar. 29/10 au wamekupanga tu uje uongeze na hayo.
Shahidi wa kificho: Tarehe 09/04 ndio maelezo yangu.
Lissu: kwahiyo huna maelezo ya ziada?
Shahidi wa kificho: Kwa hapa hamna na hayapo kwenye maelezo yangu ya Polisi.
Lissu: Najua akina Mafwele, Kingai na George wamekwambia tu kaseme sasa nakuuliza yapo maneno hayo kwenye maelezo yako ya Polisi?
Shahidi wa kificho: Unanichanganya mimi.sijui.
Lissu: Ulikaa ndani siku sita ukiwa na njaa. Hebu tuonyeshe kama yapo kwenye maelezo yako polisi?
Shahidi wa kificho: Kwa hapa hayapo ili niliyatolea maelezo.
Lissu: Kwahiyi Mapolisi wamekuuza na kukupuuza, uliwaambia vitu hawakuandika?.
Shahidi wa kificho: Kimya
Lissu: Sasa nimemaliza kukuonesha kuwa wewe ni mtu wa kupuuzwa huaminiki. Ngoja nianze kukuuliza maswali yangu sasa.
Lissu: Huo mtandao wa Facebook ni account ya nani?
Shahidi wa kificho: Ilikuwa kwenye account yangu ya faceebook.
Lissu: unaelewa kweli unachojibu? Niambie account inaitwaje?
Shahidi wa kificho: Sikujua account inaitwaje.
Lissu: Uliona video ya Tundu Lissu. Sasa Majaji hawajaona hiyo video. Wewe umewaonyesha.
Shahidi wa kificho: Simu yangu ilipotea mwaka jana.
Lissu: Umewaonyesha.
Shahidi wa kificho: Sikuwaonyesha.
Lissu: Umeiwasilisha hiyo video Mahakamani?
Shahidi wa kificho: Sikuiwasilisha.
Lissu: ulipompigia yule askari simu na kumuuliza kama wameyasikia ya Tundu Lissu. Hayo unakumbuka ulisema?
Shahidi wa kificho: Ndio nakumbuka.
Lissu: Je ulienda kutoa polisi taarifa?
Shahidi wa kificho: Sikwenda.
Lissu: Huyo ndugu yako Polisi alikwambia uende kufungua RB polisi?
Shahidi wa kificho: Hakuniambia hayo.
Lissu: Ulichosikia kwenye video kwamba kukinukisha sasa tusaidie maana ya kukinukisha ni nini?
Shahidi wa kificho: Muashirio ya kuchocheo fujo au vurugu.
Lissu: Umeyatoa wapi hayo? Mimi nina kamusi ya kiswahili. Unataka nikusomeee?
Shahidi wa kificho: Sio mbaya.
Lissu: anamsomea tokwa na harufu mbaya au vunda. Na nukia na toa harufu nzuri yakunukia kama vile marashi. Haya yakwako umetoa wapi?
Shahidi wa kificho: Mimi nimesikia mitandaoni na kupitia watu pia.
Lissu: Kwahiyo kamusi yako ni mitandao na watu?
Shahidi wa kificho: Ndio.
Lissu: Je kuna mahali kokote Polisi uliposema maana ya kukinukisha ni kufanya fujo kwenye hayo maelezo yako?
Shahidi wa kificho: Hapa Hayapo.
Lissu: Ahsante sana. Unajibu vizuri napenda.
Lissu: Waheshimiwa Majaji sina swali na shahidi..
Jaji Ndunguru anawaita Mawakili wa Serikali: Je mtakuwa na swali lolote kwa ajili ya re examination.
Ajuaye anajibu kuwa sisi hatuna swali lolote.
Jaji: Sasa shahidi tunakuruhusu tumemalizana na wewe.
Kimlango kinafungwa na Majaji wanaandika kidogo.
Anasimama Wakili wa Serikali anasema tunaomba ahirisho hadi saa nane ili tuendelee na shahidi huyo.
Lissu: Sina pingamizi ila waseme shahidi wao ni nani ili nikasome maelezo yake, kama ni wasiri waseme ni P gani pia. Nikasome ili tukirudi niwe tayari nimeshapitia maelezo yake vizuri.
Renatus Mkude Mheshimiwa Jaji tungepata ahirisho hadi kesho ingekuwa jambo jema sana, muda huu hajafika pale ofisini kwetu ndio maana tunaomba ahirisho.
Jaji Ndunguru: Jana tulielekeza, tukutane saa nane na mje na mashahidi tafadhali sana.
Kesi imehairishwa mpaka saa nane mchana.
Sehemu ya 166
Imepigwa High Courtttttt
Majaji wameingia.
Lissu alivyoingia anauliza mmekula? Mimi mwenzenu sijala kabisa.
Majaji wamewasha kipaza sauti pale na karani anasoma namba ya kesi.
Anasimama Renatus Mkude anajitambulisha na kusoma anaoambatana nao na kusema Mshitakiwa yupo.
Shauri lilipangwa na tunae shahidi P6 tuko tayari.
Lissu anasema na mimi niko tayari. Ingawa sijala mnapofunga watu mjue hilo.
Renatus Mkude anasimama anasema kula ni haki yake ya msingi kama hajala tuahirishe maana kula ni haki yake. nashangaa kwanini hajala.
Lissu anasema nimesema niko tayari maana sheria inasema mahabusu anajinunulia chakula na hela zangu wanazo wenyewe za Chakula.
Na huu ndo utaratibu wa wafungwa wote kwenye nchi hii.
Wakienda Mahakamani wanashinda njaaa. Mimi lazima niseme ili mambo haya yabadilike sio kwangu tu na kwa watu wote.
Hawa Mawakili wa Serikali na nyie majaji nafikiri mmekula mchana huu.
Huyu atakuwa ni shahidi wa tano yaani PW5 lakini jina lake ni shahidi P6 kwa Mujibu wa yale majina.
Hili jambo limewachanganya sana Majaji wanajadili kule juu sana.
Hii kitaalamu nimeambiwa inaitwa Equivocal plea yana unakubali jambo wakati umechanganya mambo humo ndani, hujakubali direct ndio maana imewavuruga.
Lissu anasema niko tayari kuendelea lakini mimi sijala.
Majaji wanaogopa.
Jaji Ndunguru: Sasa Mshitakiwa tuambie nani mwenye wajibu wa kukuletea Chakula ni akina nani? Ili tumwambie akuletee Chakula.
Lissu: Ni Magereza hawa ndio wana wajibu na Dada yangu yupo hapa wanaweza shirikiana nae.
Jaji Ndunguru: Sasa tu breki dakika 20 ili wakakupatie Chakula.
Inapigwa Courttt kesi inaahirishwa.
Wananchi walioingia Mahakamani wanawaka kinouma. Wanasema hao Magereza na serikali wanamuonea Lissu kwanini hawampi Chakula. Wakinamama wanalia sana.