Kesi 900 kwa siku 240? Hesabu zinakataa

maramia

JF-Expert Member
Jul 17, 2015
2,030
1,345
Tangu jaji mkuu Chande Othman amwambie mheshimiwa Rais kuwepo kwa mahakimu waliosikiliza na kutolea hukumu kesi zilizofikia 900 kwa mwaka, kwa namna ninavyojua matatizo katika mahakama zetu kompyuta katka kichwa changu iliyatema mahesabu hayo.

Ilinibidi nifanye utafiti mdogo kwa kuongea na marafiki zangu mahakimu wa mahakama za ngazi tofauti tofauti ili kujua uwezekano huo.

Wengi wa mahakimu niliongea nao walikiri kwamba ni vigumu sana kwa hakimu kufikia kiasi hicho cha hukumu, kwa maana ya kusoma hukumu kati ya 17-18 kwa kila wiki.

Karibu wote walisema wana utaratibu wa kusikiliza mashauri kwa siku nne na siku moja ya kusoma hukumu kwa wiki moja, na kwa kawaida kwa siku hiyo moja husoma wastani wa hukumu kati ya 6-9.

Kwa maana hiyo ukichukulia wastani huo, wastani kwa mwaka ni hukumu kati ya 310 na 470 na kwa hiyo kufika 900 walikiri ni vigumu sana. Na bado humo katikati kuna siku kuu, likizo, kuugua, safari na dharura nyingine.

Kwa hiyo kama kuna wanaotakiwa kupongezwa ama kupandishwa vyeo kwa kufikia viwango hivyo vya juu, basi ichunguzwe namna mashauri hayo yalivyoendeshwa na jinsi hukumu zilivyoandikwa isije ikawa ni ile lipua lipua mradi siku zinaenda.
 
nahisi alimaanisha zile longolongo za kahirisha kesi zipungue sasa ili kesi ziwahi kutolewa hukumu.. hesabu ya kesi 900 ni malengo lakini hesabu hiyo inaweza isifikiwe..
 
nahisi alimaanisha zile longolongo za kahirisha kesi zipungue sasa ili kesi ziwahi kutolewa hukumu.. hesabu ya kesi 900 ni malengo lakini hesabu hiyo inaweza isifikiwe..
Hapana. Usigeuze maneno ilisemwa hivi "kuna mahakimu wamehukumu kesi mpaka 900 wakati wengine wamehukumu chini ya 100..."
 
Back
Top Bottom