Kesho narudisha rasmi kadi ya CCM

Kesho narudisha rasmi kadi ya CCM

Wanajukwaa,

Nilikuwa mwanaccm miaka ya nyuma 1990_2000, nilikuja kukisusa chama hicho kuanzia mwaka 2007 kwa kuona hakikidhi yale ninayoyahitaji, tangu hapo nikaanza kutafuta upande ambao upo salama kidogo ili nishirikiane nao katika kuijenga Tanzania bora,

Mnamo mwaka 2010, Chama Cha Demokrasia na Maendeleo kilionesha ukomavu wake na ndipo nilipoanza kukiunga mkono ila sikuwa mwanachama, kwa mwaka huu nimeshirikiana nao kampeni kikamilifu na wamenifurahisha kwa kampeni safi walizofanya hasa mgombea wao wa Uraisi Mh Edward Ngoyai Lowassa,

Kwa akili zangu timamu, nikitambua umuhimu wa kuwa mwanachama kwenye chama bora, bila kulazimishwa na mtu yeyote, kesho nitaachana rasmi na Ccm na kuwa mwanachama halali wa Chadema, chini ya mwamvuli wa UKAWA.
Sitakushangaa sana wewe uliyebaki Ccm leo hii kwani kila mtu na mtazamo wake ila ninachokiamini, miaka mitano ijayo utakuwa umerudi kwenye mstari kama mimi.
Tukutane kesho jangwani.

Mungu Ibariki Tanzania.

youngsharo

Rudisha na hela ulizokula ukiwa CCM
 
Last edited by a moderator:
Wewe ni lofa akili yako ni ya kiroboto. ondoka mapema kabla tinga tinga halijatinga ikulu yambavuuuuu......
 
Umechelewa nenda saiv.kesho ndo mwisho wa toroka uje lkn nakuhakikishia baadae utataman kuomba nyingn
 
Itisha press conference kesho
 
Huhitaji elimu ya chuo kikuu kujua KANAAN mpya ilipo...ile nchi ya AHADI tutaanza kuionja tarehe 25.10.2015 UKAWA watakapokua madarakani
 
Back
Top Bottom