Mkuu
Kwakuwa mimi nakufahamu vizuri, naomba niwaaminishe watu kuwa wewe ni msomi na mbobezi wa haya mambo, hivyo pengine wachukue fursa hii kuuliza maswali ya msingi kwa wanaopenda kujifunza mambo ya ANGA.
Huyu ni Dr Jiwaji, Mkuu wa kitivo cha sayansi - Chuo kikuu Huria Tanzania
Ila mkuu, tuliojiunga na kozi ya BSc Energy Resources, wengi tumeshindwa kuendelea, imekuwa ngumu mno, hakuna usaidizi na references hakuna. Wale vijana waliochaguliwa moja kwa moja toka F6 ambao kazi yao ni shule, walifeli vibaya mitihani ya kwanza na kulazimu kuomba kufutiwa matokeo hayo.
Kila ukicheki huko duniani wanasema wana B.Eng ER, Hivi hamuwezi anzisha hizi kozi za Engineering??? Angalau wale tuliokimbia umande enzi zile tupatepo hata kadigrii ka-kustaafia.