Kesho 20/06/2017 : Mkutano wa Zuhura na mwezi Hilali {Conjuction of Venus and Crescent Moon}

Unapenda kuangalia nyota za usiku angani?

 • Ndiyo

  Votes: 6 75.0%
 • Hapana

  Votes: 0 0.0%
 • Napenda lakini sina elewa ya mambo ya anga za usiku

  Votes: 2 25.0%

 • Total voters
  8

njiwaji

JF-Expert Member
Jul 15, 2015
276
250
Alfajiri ya kesho, Jumatano tarehe 21 Juni, baada ya saa kumi na nusu utaweza kuona mkutano wa sayari ya Zuhura, inayowaka vikali sana kama nyota ya asubuhi, pamoja na hilali ya Mwezi. Zitatoa madhari ya kukvutia sana katika anga ya mashariki, kiasi cha nyuzi 40 juu ya upeo wa mashariki Jua linapochomoza.


The dawn of Wednesday from 4:30 AM on 21 June will provide a spectacular show of a crescent Moon that is very close to brilliant Venus. The beautiful sight will be seen in the east, 40 degrees above the eastern horizon when the Sun rises.

Zuhura na Mwezi Hilai zakutana.jpg
 

demigod

JF-Expert Member
Jan 2, 2015
5,689
2,000


Inawezekana sisi kwa Tanzania kuweza kuuona?

Tutatumia macho ya nyama au Darubini?
 

njiwaji

JF-Expert Member
Jul 15, 2015
276
250

Inawezekana sisi kwa Tanzania kuweza kuuona?

Tutatumia macho ya nyama au Darubini?
Haya niliyoandika ni kwa watazamaji wa Tanzania. Mimi huwa ninaeleza vitu tunavyoweza kufaidi sisi wenyewa na kueleza muda gani na upande gani kugangalia hapa kwetu Tanzania.
 

njiwaji

JF-Expert Member
Jul 15, 2015
276
250
aseeh haya mkuu ila ningekuwa na kitelescope ningeona mubashara
Ni kweli, ukiwa na darubini (telescope) utaona hali ya sura ya Mwezi na pia umbo la Zuhura ambayo haipo duara kamili ni duara pungufu kidogo.

Lakini hata kwa macho ni kitu pekee kuona hivi vitu vikiwa karibu kiasi hiki. Siyo kawaida.
 

Joseverest

Verified Member
Sep 25, 2013
44,074
2,000
Ni kweli, ukiwa na darubini (telescope) utaona hali ya sura ya Mwezi na pia umbo la Zuhura ambayo haipo duara kamili ni duara pungufu kidogo.

Lakini hata kwa macho ni kitu pekee kuona hivi vitu vikiwa karibu kiasi hiki. Siyo kawaida.
ok sawa mkuu
 

BIGstallion

JF-Expert Member
Sep 13, 2016
6,364
2,000
Maana ni kufaidi mandahari na kujua kuwa vitu hivi vinasogea sogea angani. Sayari na Mwezi hutembea angani kwa vile zipo jirani na sisi, ila nyota hazisogei kwa vile zipo mbali mno mno.

Sawa mnajimu nimekuelewa,
 

Ndalilo

JF-Expert Member
Jan 30, 2013
1,457
2,000
Mkuu

Kwakuwa mimi nakufahamu vizuri, naomba niwaaminishe watu kuwa wewe ni msomi na mbobezi wa haya mambo, hivyo pengine wachukue fursa hii kuuliza maswali ya msingi kwa wanaopenda kujifunza mambo ya ANGA.

Huyu ni Dr Jiwaji, Mkuu wa kitivo cha sayansi - Chuo kikuu Huria Tanzania

Ila mkuu, tuliojiunga na kozi ya BSc Energy Resources, wengi tumeshindwa kuendelea, imekuwa ngumu mno, hakuna usaidizi na references hakuna. Wale vijana waliochaguliwa moja kwa moja toka F6 ambao kazi yao ni shule, walifeli vibaya mitihani ya kwanza na kulazimu kuomba kufutiwa matokeo hayo.

Kila ukicheki huko duniani wanasema wana B.Eng ER, Hivi hamuwezi anzisha hizi kozi za Engineering??? Angalau wale tuliokimbia umande enzi zile tupatepo hata kadigrii ka-kustaafia.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom