Kero za wapiga debe stand za mabasi

Kero za wapiga debe stand za mabasi

de98

JF-Expert Member
Joined
Aug 13, 2017
Posts
737
Reaction score
760
Heshima ziende kwenu wakuu,

Hivi nanyi huwa mnakutana na kero za wapiga debe al maarufu kwa jina saranga.

Wapiga debe wa hapa Magufuli stand kiukweli wamekua kero mno hawana tofauti na boda boda ukimuangalia usoni tu huyo alishakuja kukushika nguo akijua ni abilia.

Hatukatai kuwa nao wanatafuta riziki lakini njia ya utafutaji imekua kero mno kwa sisi ambao huwa tunapita mazingira ya darajani juu kuwahi usafiri makazini asubuh na jioni au kwenye mishe mishe zingine tu pembezoni kwa stand iyo.

Njia ipi mdau unadhani ni sahihi kwao katika utaftaji riziki ili hata tunapowajibu isiwe kwa ghazabu, nawasilisha.
 
Daah naona leo mnatuandama sisi watu wa mbezi aisee mnataka tukale wapi ....? Asubuh mpka jioni napiga debe jioni naingia kwenye kitengo cha kuuza supu apo mbezi chini stand ya kinyrezi
 
Wanapenda kupiga vya juu , wanapenda kuwafanya watu wajinga duh
 
Daah naona leo mnatuandama sisi watu wa mbezi aisee mnataka tukale wapi ....? Asubuh mpka jioni napiga debe jioni naingia kwenye kitengo cha kuuza supu apo mbezi chini stand ya kinyrezi
Mnakera aisee riziki haitafutwi kwa kuvunjiana heshima huko tena mkikuta mtu mgeni wa mji ndio mnamsumbua mno na kumuibia juu
 
Nimekutana na mmoja mstarabu kweli ,kaniuliza Kama nasafiri nikamjibu hapana,akaniuliza unaingia stend kwa ajili ya huduma gani?nikamjibu nafuata mzigo,ofisi nilikua siijui akanipeleka ,Bila kudai ata kumi,akaniambia siku nikisafiri nimcheki,tukapeana tano akasepa
 
Mnakera aisee riziki haitafutwi kwa kuvunjiana heshima huko tena mkikuta mtu mgeni wa mji ndio mnamsumbua mno na kumuibia juu
Ila mimi sio mwizi mkuu wajinga wajinga wasio waadilifu ndo hufanya hvo wahuni wapo kila sehemu
 
Nimekutana na mmoja mstarabu kweli ,kaniuliza Kama nasafiri nikamjibu hapana,akaniuliza unaingia stend kwa ajili ya huduma gani?nikamjibu nafuata mzigo,ofisi nilikua siijui akanipeleka ,Bila kudai ata kumi,akaniambia siku nikisafiri nimcheki,tukapeana tano akasepa
Jinsia yake tafadhalii...
 
Hii kazi ni moja ya Kazi inayodhihilisha Umaskini wa Nchi hii.
 
Kuna Mmoja Alinipokea Kistaarabu Akanipa Seat No : A1 Mtei BBT-DSM, Asubuh Naenda Naambiwa Basi Ketu Halina Herufi Lina Namba Tu 1,2,3 Kwahiyo Nikae Seat Ya Mwisho! Nikasema Hapana Nikawauliza Huyu Mtu Mnamjua Maana TIN Number Ni Yenu Wakanisema Ndio Tusamehe! Nikasema Hapana Nikaenda Kukaa Siti Ya Kwanza Mweny Siti Kaja Nikamkazia Huku Nimeshika Simu Na Rekod Matukio Yote! Nikawaambia Leo Nitawafurahisha! Final Nikasafir Kwa Seat No 2 Na Mikwara Kibao
 
Back
Top Bottom