Kero ya Meseji za Usajili wa Simu!

BOB LUSE

JF-Expert Member
Jan 25, 2014
3,558
2,854
Simu yangu, Mbona Tunakumbushana kutwa mara tatu nisajili Laini kwa alama za vidole.HILI NI JAMBO LA HIARI LISIWE KERO Kama Sasa hivi!

ONYO! LAINI YAKO ITAFUNGWA BAADA YA 31/12/2019 IKIWA HAIKUSAJILIWA KWA ALAMA ZA VIDOLE. Tembelea duka la Tigo au Wakala ukiwa na NAMBA YA NIDA AU KITAMBULISHO
 
Kitambulisho cha uraia sina
Halafu sijishugulishi kukipata, nangoja serikali ije inipige picha iniletee kitambulisho nyumbani. Namba yangu sijaombea kazi mahala wala sina biashara kusema wateja watanitafuta.Sifungui sanduku la posta,ikifika tarehe1 wafunge tu hizo line ili nipate akili ya kwenda kufagia hospitali au kuuza maji road
 
Wanakera unakuta una simu ya haraka kuongea, ukipiga Wana leta sauti ya maelezo kuhusu usajili nusu dakika nzima
 
Simu yangu, Mbona Tunakumbushana kutwa mara tatu nisajili Laini kwa alama za vidole.HILI NI JAMBO LA HIARI LISIWE KERO Kama Sasa hivi!

ONYO! LAINI YAKO ITAFUNGWA BAADA YA 31/12/2019 IKIWA HAIKUSAJILIWA KWA ALAMA ZA VIDOLE. Tembelea duka la Tigo au Wakala ukiwa na NAMBA YA NIDA AU KITAMBULISHO
wacha maneno nenda kasajili line Mara moja
 
Halafu sijishugulishi kukipata, nangoja serikali ije inipige picha iniletee kitambulisho nyumbani.

Nimecheka bila kujipanga😂😂😂
Ungekuwa jirani yangu ningekuwa sikauki kwako maana umeniongezea siku za kuishi
 
Kafanye hilo Zoezi uone kama watakukera
Sasa hivi kusajili haichukui hata dakika mbili aende kwa mawakala wako kibao na vimashine vyao mitaani dakika mbili haziishi ushasajiliwa .Sijui kwa Nini watanzania wengine ni wazito.
 
Sasa hivi kusajili haichukui hata dakika mbili aende kwa mawakala wako kibao na vimashine vyao mitaani dakika mbili haziishi ushasajiliwa .Sijui kwa Nini watanzania wengine ni wazito.

Kuna shida kubwa ya mtandao kwa baadhi ya maeneo, nikiwa pale Mwenge Jumanne kijana mmoja anamshawishi binti asubiri mpaka jioni mtandao ukirudi♧♢♡♤
 
Kuna shida kubwa ya mtandao kwa baadhi ya maeneo, nikiwa pale Mwenge Jumanne kijana mmoja anamshawishi binti asubiri mpaka jioni mtandao ukirudi♧♢♡♤
Huyo atakuwa alikuwa akimtaka binti wa watu wakutane gizani
 
Vodacom Tanzania, mimi nimesajili kwa alama za vidole lakini wiki hii mmeanza kunikumbusha tena nikipiga simu tu mnaanza kunikumbusha ina maana usajili wangu mmeufuta au?!
 
Back
Top Bottom