Kero ya Huduma za Bima ya Afya MOI

Mzee wa Gwata

Member
Apr 11, 2017
20
6
WanaJF.

Natumai mubukheri wa afya. Napenda kutoa masikitiko yangu kutokana na utaratibu mbovu wa huduma za Bima ya Afya za NHIF katika hospital ya Muhimbili kitengo cha mifupa Almaarufu MOI.

Maafisa wanaokusanya kadi za Bima ya Afya baada ya matibabu inamchukua mgonjwa SAA 1 hadi SAA 2 kupewa kadi yake baada ya kupatiwa matibabu.

Mbaya zaidi mgonjwa akiwauliza mbona kadi yangu sipewi nirudi nyumbani wana maneno machafu sana kwa wagonjwa.

Binafsi hata Leo nimetoka chumba cha mazoezi tangu SAA 3 kamili lakini hadi sasa SAA 4.13 bado niko hapa kwenye benchi nasubiri kadi yangu.

Wiki iliyopita nilijibiwa kuwa kwani umeletwa hapa si uende nyumbani," kadi kadi tumechoka". Sasa leo nimeona nibaki kimya niseme na keypad ya simu yangu labda wahusika watatusaidia.

Waheshimiwa Kigwangalla na Ummy kazi mnayo
 
Back
Top Bottom