PeaceLover
Member
- Oct 21, 2012
- 7
- 1
Inawezekana kabisa foleni tunayokutana nayo hapa mjini si kwa sababu eti barabara ni nyembamba tu hapana!
Kuna mambo kama vile wasimamia sheria za barabarani (Traffic police) kutojipanga vema kuweka utulivu kwenye barabara zetu. Mfano ukiwa katikati ya mji utawakuta traffic wamekaa kona hata wa4 au zaidi wakati sehemu zingine za pembezoni kidogo ya mji kama vile mbagala, kimara, mbezi, tegeta nk. ambako ndiyo kwenye vurugu zaidi HAWAPO kabisa! Suala lingine ni ukosefu wa uvumilivu kwa madereva wasiokuwa na busara za kazi yao. Utakuta barabara ina lane 1 ya kwenda na 1 kurudi, sasa mkiwa kwenye foleni kuna wajanja (mi nawaita wajinga tu) wanachomoza na kupita kwenye lane inayopaswa kutumika kwa magari yanayotoka upande wa pili na kwenda kuchomeka mbele ya wenzao huku wakiwa wamefunga njia ya upande mwingine! Jamani huu ni UJINGA wa aina yake.
Rai yangu ni kwamba:
1. Jeshi la polisi lihakikishe linasambaza askari wa kutosha barabarani ili kukabiliana na madereva wajinga wanaofunga njia na kusabaisha msongamano usiokuwa wa lazima.
2. Madereva mzingatie taaluma zenu na kuwa na busara zaidi hasa ukifikiria watu wote wanaharaka ya kufika waendako.
Karibuni wadau kuchangia hoja.