Kero namba moja mwendo kasi

Kero namba moja mwendo kasi

Tyupa

JF-Expert Member
Joined
Aug 11, 2013
Posts
802
Reaction score
657
Mlundikano wa kutisha wa abiria Kimara mwisho unasababishwa na wahusika makusudi ili waweze kujipatia pesa zaidi.Ni jambo la ajabu sana kuwabeba abiria waliojazana Mbezi Luis ambao karibu wote safari yao ni kwenda mjini lakini wote huishia kumwagwa Kimara mwisho.Baada ya kumwagwa hapo huanza upya kutafuta magari mengine ya kwenda mjini.Na wale waliotoka mjini ambao mwisho wao ni Mbezi hushushwa Kimara mwisho pia ambapo nao huanza upya kutafuta magari mengine ya kwenda Mbezi Luis.Ni magari yale yale tena huanza kuhangaika kuwasomba kuwapeleka Mbezi au mjini.Ni maajabu ya dunia wakati serkali inatafuta sababu na dawa ya kuboresha usafiri wa mwendokasi akiwemo Makonda mwenyewe kero hii HAIONWI na yeyote yule.Uwezo wa kupunguza msongamano pale Kimara mwisho ni kuwabeba abiria moja kwa moja kutoka Mbezi Luis hadi mjini bila ya kuwashusha wote Kimara. Na wale wanaotoka mjini kwenda Mbezi hakuna haja ya kushusha wote Kimara mwisho na baadae tena waanze kutafuta tiketi nyingine kwenda huko.Tunajua wahusika wanahangaika na sh 400 wanayotoza kwenye hii ruti ndogo . Kama tatizo ni pesa basi serkali iwaongezee nauli ili waache mchezo wakuwalundika abiria Kimara na kusababisha usumbufu mkubwa na kupoteza muda.
 
Poleni sana abilia mnapita njia hiyo
 
Leo tena msongamano wa abiria Kimara mwisho umeleta kizaza cha aina yake baada ya magari kuwa machache.Sababu kubwa ya msongamano huo ni kama nilivyoeleza mwanzo.Makonda anapaswa kuingilia kati kuzuia kusomba abiria kutoka Mbezi Luis na kuwashusha Kimara.Na wale wanaotoka mjini kwenda Mbezi wasisushwe Kimara.Bila kufanya hivyo huo msongamano hautaisha milele.
 
Back
Top Bottom