A
Anonymous
Guest
Habari, nina malalamiko kuhusu ndugu zetu wa NSSF Mkoa wa Mtwara, hasa Wilaya ya Masasi.
Kuna baadhi ya watumishi waliokuwa wakifanya kazi katika Kituo cha Afya Rehema, Newala, ambao walikuwa wanakatwa fedha zao za NSSF. Hata hivyo, baada ya kuondoka kazini Mwaka 2023, hadi leo (Septemba 2026) hawajapata fedha zao, huku baadhi yao wakifariki bila kupata stahiki zao.
Baadhi ya ndugu zangu wamefika hata kwa Mwanasheria wa Wilaya, lakini wanapowasiliana na watumishi wa NSSF hakuna hatua zinazoonekana kuchukuliwa. Watu wanatumia fedha zao kusafiri kutoka Newala kwenda Masasi, lakini wanarudi bila majibu ya maana.
Afadhali meneja wa zamani wa NSSF alikuwa akifuatilia suala hili na watu walikuwa wakipata fedha zao, lakini kwa meneja wa sasa hakuna kinachoonekana kufanyika. Ndugu zetu, akina mama na dada zetu wanaendelea kuteseka.