Mkulima wa Kuku
JF-Expert Member
- Jan 13, 2011
- 1,270
- 534
Kero maji Dar kuanza kutoweka mwezi ujao.
NA FRANK MONYO
3rd March 2016
B-pepe
Chapa
Sina hakika wanapozungumzia Dar pia wanawaza maeneo kama Mbagala ambako haijawahi kutokea miundo mbinu ya maji ya DAWASCO ikawepo. Nadhani wanazungumzia wanakoishi binadamu "wenye nchi" lakini sina hakika kama wanazungumzia kwa "wananchi". Inawezekana wanadanganywa viongozi kuwa ni pamoja na kwa "wananchi" na kwa kuwa viongozi hawawezi kuja waliko "wananchi" basi inakula kwetu. Sisi na maji ya visima na maji ya visima na sisi
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Mecky Sadiki.
Wakazi wa Jiji la Dar es Salaam wanaohudumiwa na mtambo wa Ruvu Juu, wanatarajia kuondokana na kero ya maji baada ya mradi wa ujenzi wa tangi kubwa la kuhifadhia maji kukamilika mwishoni mwa mwezi huu.
Ujenzi wa tangi hilo lililopo eneo la Kibamba jijini Dar es Salaam, umekamilika kwa asilimia 90 na litakuwa na uwezo wa kuhifadhi lita milioni 10 za maji ambapo litakuwa na uwezo wa kuhudumia wateja 500,000 kwa siku.
Akizungumza katika ziara ya kukagua mitambo ya Maji Ruvu Juu na Chini, Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi, alisema mtambo wa kusukuma maji kuingiza katika tangi hilo, unatarajiwa kuwashwa mwanzoni mwa Aprili, mwaka huu.
Alisema wakazi wa Jiji la Dar es Salaam watarajie kupata maji ya uhakika kwani kazi ya ujenzi ya tangi hilo imefikia hatua za mwisho.
Ziara hiyo iliyofanywa na Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Dar es Salaam (RCC) ikiongozwa na wabunge wa mkoa huo, mameya na wakurugenzi wa manispaa zote kwa lengo la kukagua miradi ya maji inayoendelea.
Mushi aliyemwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Mecky Sadiki, alisema watu wanaoishi karibu na mabomba makubwa na vyanzo vya maji, wanapaswa kuvilinda ili wasiathiri upatikanaji wa maji.
“Tatizo la maji litakuwa historia katika Jiji la Dar es Salaam maana mradi huu ni mkubwa sana na utawezesha watu wengi kupata huduma ya maji safi na salama," alisema.
Mushi aliongeza kuwa hata baadhi ya yale maeneo ambayo yalikuwa hayapati maji kwa kipindi kirefu, yatapatiwa huduma hiyo kutokana na kukamilika kwa ujenzi wa tangi hilo.
Hata hivyo, aliwahimiza wananchi kuhakikisha kwamba wanajenga utamaduni wa kulipa ankara za maji kwa wakati na kuachana na tabia za wizi wa huduma hiyo kwani kwa kufanya hivyo kunasababisha hasara kwa serikali na hivyo kushindwa kuboresha miundombinu.
Mkurugenzi wa Usimamizi na Ufundi wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka (Dawasa), Romanus Mwang’ingo, alisema tangi hilo litahudumia wakazi wa maeneo ya Kiluvya, Kimara, Mbezi, Segerea, Kinyerezi, Ubungo, Kibangu, Tabata na Kibamba.
Aidha, alisema mkandarasi wa kusambaza mabomba kwa wananchi, tayari amepatikana na anatarajiwa kuanza kazi muda wowote kuanzia sasa.
Kwa upande wake, Mbunge wa Viti Maalum Jimbo la Ilala kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Anatropia Theonest, alitoa wito kwa Dawasa kuhakikisha wanatekeleza kwa wakati mradi wa kuunganisha mabomba kwa wananchi ili kwenda sambamba na wingi wa maji yanayotarajiwa kuongezeka.
Aidha, aliishauri Dawasa kutumia vyanzo mbadala vya kuzalisha umeme wa takataka katika mitambo ya Ruvu Juu na Chini ili kupunguza gharama iliyopo sasa ya matumizi ya umeme wa Shirika la Umeme nchini (Tanesco).
“Tunaweza kutumia umeme wa takataka kusukuma mitambo yetu ya maji badala ya kutumia umeme wa Tanesco ambao ni ni wa gharama na hivyo kuongeza ufanisi, ” alisema.
Desemba 31, mwaka jana, Serikali ya Tanzania na India zilisaini mkataba wa ufadhili wa Dola milioni 59.3 kwa ajili yha utekelezaji wa mradi wa ulazaji wa bomba la maji kutoka Mlandizi hadi Kimara na Kinyerezi pamoja na ujenzi wa tangi la kuhifadhia maji eneo la Kibamba.
CHANZO: NIPASHE
Habari Zaidi
Articles
Yanga ijipange kuing'oa APR Afrika.
Kinara uporaji benki Mbagala mbaroni.
Mbowe amshitaki Magufuli kwa maaskofu.
Majaliwa anusa harufu ya ufisadi Bandari Mtwara.
Halmashauri Tanga hatarini kuvunjwa.
Walimu Dar kusafiri bure.
Magufuli uso kwa uso na Nkurunziza, Museveni.
Nitashinda urais uchaguzi wa maruidio Zanzibar'