Abdul Nondo7
Member
- Feb 22, 2017
- 9
- 25
Kwako Mh. Naibu waziri wa afya, Dr. Hamis Kigwangala, habari za majukumu natumai unaendelea vyema na majukumu yako ya kila siku ya kutumikia watanzania, mungu aendelee kukupa afya njema na uwajibikaji uliotukuka.
Taarifa zilizopo ni kuwa hospital ya MUHIMBILI kitengo cha mifupa (MOI).wagonjwa wa kitanzania wanateseka, wanaumia na wengine wanakufa sababu ya kutopata matibabu mwezi sasa, wagonjwa wenye matatizo ya mgongo wanaohitaji upasuaji tangu January hadi sasa machi hawajapatiwa matibabu yeyote, sababu zinazotolewa ni kuwa kitanda cha upasuaji mgongo (TABLE 5) kimeharibika mwezi na nusu sasa.
Jambo linalopelekea wagonjwa kuendelea kuteseka na wengine kuumia na hata wengine kufa, na taarifa zilizopo mkurugenzi anafahamu lakini hana ushirikiano wowote, Jambo linalopelekea foleni ya wagonjwa kuwa kubwa, na kuendelea kuteseka. Nimeshuhudia leo mama akiwa na mtoto wake akilalamika kuwa mtoto wake hali inazidi kuwa mbaya alikuwa afanyiwe upasuaji tangu decemba ila kitanda cha upasuaji mgongo (TABLE 5) kimeharibika, bila hatua yeyote kuchukuliwa na Mkurugenzi othuman kilolomo tatizo hili analijua bila hatua yeyote kuchukuliwa.
Tunakuomba Mh. Naibu Waziri Hamisi Kigwangala kuchukua hatua ya haraka juu ya Jambo hili ili kuokoa watanzania wanaohitaji matibabu, na upasuaji uendelee Kama kawaida.
Shukrani Mh. Waziri natumai utachukua hatua za haraka, kuondoa tatizo hili.
Wako mtiifu,
Abdul Omar Nondo.