Kuna barabara iendayo Makao Makuu ya Ilemela kupitia karibu na Msikiti wa Waislamu, Gedeli Guest House, Shule ya Msingi Gedeli na kuendelea ni kero KUBWA sana kwa wananchi wanaoishi kando kando ya barabara hii kama ifuatavyo:-
- Vumbi nyingi inayotimuliwa na magari mengi ynayopita kwenye barabara hii.
- Ugonjwa wa mara kwa mara kutokana na vumbi hasa watoto.
- Kelele nyingi kutokana na magari na hivyo kutunyima usingizi.
- Uchafu unaoletwa na vumbi ya magari na hivyo kutupa gharaz kubwa.
- Wageni wengi kukimbia nyumba za kulala wageni kutokana na kelele za magari na vumbi.