Kenyatta- Watanzania iombeeni Afrika Mashariki | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kenyatta- Watanzania iombeeni Afrika Mashariki

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by mdau wetu, Nov 7, 2011.

 1. m

  mdau wetu JF-Expert Member

  #1
  Nov 7, 2011
  Joined: Apr 20, 2011
  Messages: 548
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  NAIBU Waziri Mkuu wa Kenya, Uhuru Kenyatta amewataka Watanzania kuiombea Jumuiya ya Afrika Mashariki ili kukabiliana na matatizo yaliyo mbele yake.

  Alisema bila msaada wa nguvu za Mungu ni vigumu kupata utatuzi wa matatizo yaliyo mbele ya jumuia hiyo kwani ni kikwazo cha maendeleo.

  Akizungumza jana wakati wa ibada ya Mavuno katika Kanisa La Mtakatifu Joseph, Kenyatta ambaye pia ni Waziri wa Fedha, alisema msaada wa Mungu na juhudi za kila mmoja zitasaidia kutatua matatizo yaliyo mbele na kuinua uchumi wa wananchi wa jumuia hiyo.

  Alisema kila mmoja kwa wakati wake anatakiwa kutenga muda wa kuombea jumuiya hiyo aliyosema inayokabiliwa na matatizo mbalimbali, ili Mungu awape busara viongozi wake katika kuyatatua.

  Uhuru alisema yuko nchini kuhudhuria kikao cha masuala ya jumuia hiyo na katika ibada hiyo, aliambatana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bernard Mambe na Balozi wa Kenya nchini, Mutindo Mutiso.

  Kenyatta pia alichangia Kwaya Kuu ya Mtakatifu Joseph Dola 200 kwa ajili ya safari ya kuhubiri Injili watakayofanya Mombasa nchini Kenya kuanzia Novemba 18 mwaka huu.

  Ibada hiyo iliongozwa na Padre Camilius Sawio aliyetaka waumini kutoa mavuno yao na kuomba hekima na busara kwa Mwenyezi Mungu ili kuweza kutatua masuala mbalimbali ya kimwili na kiroho.

  Paroko Msaidizi wa Kanisa hilo, Edwin Igomba alisema kanisa hilo lina wajibu na nafasi kubwa kuomba kwa ajili ya nchi hususani kwa waliopotoka katika masuala mbalimbali.
   
 2. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #2
  Nov 7, 2011
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Anamjua Mungu siku zote au wakati wa shida tu?
   
Loading...