Kenyatta awashiwa taa ya kijani kuwania awamu ya pili, awataka wakenya kukubali matokeo

Majs

JF-Expert Member
Dec 21, 2012
232
497


Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta ameidhinishwa na mamlaka ya uchaguzi ya Kenya kugombea Urais pamoja na mgombea mwenza, William Rutto. Kenyatta ametaka wote kukubali hukumu itayotolewa na wakenya siku ya uchaguzi, amesema Kenya ipo kabla ya uchaguzi na itakuwepo baada.

Ameahidi tume na wakenya kuwa chama cha Jubilee kinasimama kwa ajili ya amani, umoja na maendeleo ya wakenya wote. Amesisitiza wanajipangaa kuhakikisha wanafanya uchaguzi kwa amani wakiamini ni wakenya wenye haki ya kuchagua viongozi wao na wataheshimu mapendeleo yao.

Amewaomba wakenya kukipa chama chake cha Jubilee nafasi nyingine ya kuwaongoza na kuendeleza kazi waliyoianza.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom