Kenyatta aahidi elimu bure Kenya

Dam55

JF-Expert Member
Oct 8, 2015
5,641
11,957
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta alitoa ahadi ya kutoa elimu bure kwa wananchi wa kenya.
Alitoa kauli hiyo Jana wakati akijinadi mbele ya raia wa kenya.
Alisema iwapo atapata nafasi hiyo kwa awamu ya pili atatoa elimu bure kuanzia shule ya msingi hadi kidato cha NNE. (O' level)
 
Anaiga nyayo? hivi amefanya utafiti na kuona jinsi ya kurekebisha makosa? Elimu bure ni janga akikurupuka
 
MAMBO MAGUMU BADO
 
ugumu wake nini?????mbna watoto hapa TANZANIA wanasoma vizuri tu?????
TATZO LENU MNSTAKA KUSIKIA MABAYA TU JUU ELIMU BURE......na hili msahau kabsa
Mkuu kwani Mimi nimesema kuna baya hapo?
 
Anaiga nyayo? hivi amefanya utafiti na kuona jinsi ya kurekebisha makosa? Elimu bure ni janga akikurupuka

Wapi tumeiga, mbona elimu ya Kenya ni bure, kuanzia darasa la kwanza hadi la nane.
Alichoahidi Uhuru ni elimu ya sekondari ambayo anataka kuifanya iwe bure.
 
Tulikumbana na changamoto alipoanzisha Mwai Kibaki, lakini taratibu tumeendelea kuboresha.

Hebu nambie, shule hizo za bure zinapata ruzuku toka serikalini? kwa wakati? ya kutosha? zinafanya vizuri? Walimu hawana malalamiko?
 
Siasa bwana, wakati Mwalimu akitoa elimu bure walisema eti ni ujamaa sasa nao wanaelekea huko huko! Kibaya zaidi waliomkashifu Mwalimu wengine wako hapa hapa na walijilinganisha na Kenya! R.I.P Mwalimu.

cc: Waliobinafsisha elimu!
 
ugumu wake nini?????mbna watoto hapa TANZANIA wanasoma vizuri tu?????
TATZO LENU MNSTAKA KUSIKIA MABAYA TU JUU ELIMU BURE......na hili msahau kabsa
elimu bure ambayo haina kiwango kila siku mnabadili mitaala,mtoto anamaliza la saba bila kujua kusoma na kuandika ujinga kama huu hapa chini ndio mafanikio ya elimu bure
upload_2017-5-18_11-38-20-png.510968
upload_2017-5-18_11-39-36-png.510970
 
Hebu nambie, shule hizo za bure zinapata ruzuku toka serikalini? kwa wakati? ya kutosha? zinafanya vizuri? Walimu hawana malalamiko?

Leo hii tunaongea mambo ya watoto kupewa laptops za bure kila wanapoingia shuleni.
Bajeti kwa ajili ya elimu ya bure 2014/2015 ilikua Kshs 40b (TZS 920B).
Mitihani ya kitaifa yaani, ya msingi KCPE na ya sekondari KCSE ni bure hailipiwi tena.
Wanafunzi wanaojiunga na hizi shule wameongezeka kwa asilimia 10% tangu 2013.

Halafu walimu Kenya hulipwa na serikali sio shule, mwalimu wa shule ya msingi wa kiwango cha chini analipwa TZS 600,000
Na kwenye mitihani ya kitaifa, tunaona shule za umma zinafanya vizuri sana.
 
Back
Top Bottom