Kenya's Day of Pride; The Birth of a New Republic

Sasa ni zamu ya Eric Waina ina anaimba wimbo wake maarufu.....wa kuisifia Kenya, "daima mimi mkenya"


Huo wimbo wake umetumika kwenye mojawapo ya jingo za matangazo ya kampuni mojawapo ya simu, sijui ni ipi imenipita kiodogo
 
tKweli tunahitaji kukaa chini nakulifanyia kazi, chamgamoto ni je tunao watu wenye kuthubutu kutoa changamoto ya kweli..kumbuka kenya imewachukua miongo 2 ya hata kumwaga damu kufika hapo walipo leo. Natumaini kwa sifa yetu ya amani na upeo na busara za viongozi wetu tunaweza kufikia hapa wakenya walipofikia leo hii kwa amani kabisa!:smile-big:

Hapo kwenye redi yataka moyo mkuu!
 
Sasa ni zamu ya State House Choir....tunaambiwa hii choir imekuwa formed na facilitated by Lucy Kibaki
 
Sasa anaongea Hon, Kalonzo Mosyoka, VP........anamwita Raila 'my brother and Prime Minister' watu wanashangilia sana....
 
Hapo nazani wanatuzengua tu. Lucy Kibaki ajua wapi kuimba tena?


Ndo hapo sasa nadhani ni katika kuweka mazingira mazuri ya kufanya kazi kwa state house staff...LOL

mi ningependa kujua kama kale katoto ni kajukuu ama nini? manake kaja nako kwenye limosine.....nadhani kama 8-9 years
 
sasa Raila Odinga anaanza kuongea.....kila anapoweka nukta anashangiliwa sana na umati wa watu waliofika!
 
"The 4th of August will go down in History"....I hope ame acknowldge source lol
 
Anamsifia Mwai Kibaki......kwamba "aliresign from the government in 1992 and never looked back...20 year later ameiongoza nchi kwenye katiba mpya" (tafsiri yangu)

Anamsifia Koffi Annan, Benjamin Mkapa na Graca Machel, ambao walikuwa nao bega kwa bega wakati wa majaribu,
 
"The New constitution has set us free" (Raila Odinga, 27th August 2010)

"Miaka imezaa miezi, miezi ikazaa wiki, wiki ikazaa siku na siku ikasaa masaa, na saa ni sasa, katiba ni SASA" (hapo anaongea Kiswahili na anashangiliwa sana na wananchi)
 
Anaongeza........"Utawala wa Imla na Kimabavu umewekwa kwenye kabiuri la sahau,, Mafirauni warudi kwao...."

Kitendawili!....yeye ni mnyama na yeye ni ndege, ni nani? wanajibu Popo" sijui anamaanisha nini LOL
 
"Mwishowe sasa wamemwita ndumilakuwili.......sikujua kama jamaa ana mipasho hivi....."

Wakenya wamesema kwa heri kwa POPO.....

Anamshukuru Mwai Kibaki (tena)....anamfananisha na Iniesta, yeye Odinga Fabregas,, LOL
 
Mwai Kibaki anaongea sasa...


Sasa naona tumewakilishwa na 'His Excellencey Aman Karume, President of Zanzibar'...hivi Tanzania Imekufa ? au haijawahi kuwepo
 
Back
Top Bottom