Bowie
JF-Expert Member
- Sep 17, 2016
- 4,373
- 6,084
Uchimbaji mafuta unaanza kuchimbwa rasmi mwezi wa sita mwaka huu huko Kenya. Kampuni ya Tullow Oil ndio imeingia mktaba na serikali ya Kenya katika uchimbaji wa mafuta hayo. Baada ya serikali ya Kenya kuunda tume mwaka 2013 iligundulika serikali ya Kenya itapata mgao wa Dola za kimarekani bilioni moja na nusu kwa mwaka ambazo fedha hizo zitapelekwa mojamoja kwenye hazina kuu ya serikali hiyo ya Kenya.
Hapa Tanzania pamoja na gesi nyingi kugundulika huko kusini lakini hakuna uwazi wowote umewekwa kwenye mikataba hiyo na ripoti ya CAG imesema hivyo.
Kwa maslahi ya taifa hili ni wajibu wa serikali ya awamu ya tano kuangalia upya mikataba ya uchimbaji wa gesi hiyo ili watanzania wajue mchango wa gesi hiyo kwenye pato la taifa na hata ikiwezekana kuvunja mikataba hiyo kwa maslahi ya taifa. Tusipoangalia Tanzania inaweza kufuata njia ya Nigeria kuwa ni nchi inayotoa mafuta kwa wingi Afrika lakini ndio umasikini ni mkubwa sana,
Serikali awamu ya tano imekuwa makini sana kwa ukusanyaji wa kodi kutoka kwa wafanyabiashara wazawa itakuwa sio kuwatendea haki kuacha makampuni ya nje yaendelee kutupora maliasili yetu kwa kutumia jina la uwekezaji.