Kenya: Mzee azikwa akiwa ameketi

Kenya: Mzee azikwa akiwa ameketi

figganigga

Platinum Member
Joined
Oct 17, 2010
Posts
26,699
Reaction score
59,210
141026104005_jeneza_la_kuketi_512x288_bbc.jpg

Picha kwa niaba ya gazeti la standard nchini kenya


Je,katika utamaduni wenu kiongozi wa kijiji,mganga wa kienyeji na mkulima mashuhuri huzikwa vipi?.

katika kisa cha kushangaza ,wana kijiji wa Eshikombelo katika kaunti ya kakamega nchini kenya wanasema kuwa iwapo marehemu angekuwa mzee Adriano Aluchio angefanyiwa maziko ya kipekee.

Kulingana na gazeti la Standard nchini kenya,maelfu ya wanakijiji wa eneo hilo walihudhuria mazishi ya marehemu Aluchio ili kumpa heshima yake ya mwisho mzee huyo wa miaka 62.

lakini wengi wao walitaka kushuhudia sherehe ya kipekee ya Idakho.
Watu wa makabila madogo ya Bukusu,Idakho,Tachoni na Kabras katika kabila la Waluhya wanaamini kwamba kuwazika watu mashuhuri wakiwa wameketi ni ishara ya heshima kubwa sana.

''Tulipata tamaduni hizi na hivyobasi ni sharti tuishi nazo'' alisema Mzee Museve Mwidakho.
Mwidakho ambaye ni mzee wa ukoo wa kabila dogo la Idakho ambako marehemu Aluchio anatoka anasema kuwa utamaduni huo unalenga kuwashirikisha wafu na watu walio hai.

Anasema kuwa utamaduni huo ulianzishwa na Nabongo Mumia wa jamii ya Wanga na hadi leo umeigwa na makabila mengine madogo.
Anasema kuwa kumzika mtu akiwa ameketi pia kunafukuza mapepo wachafu. Mia

Chanzo: BBC
 
Kwetu Mara nyingi waganga ndio wanazikwa hivyo, lakini sio hawa waganga matapeli hao ni waganga asilia.!
 
Mazishi ya aina hiyo ni ya kawaida sana kwa wazanaki. Juzi tu, mzee marwa ihunyo kazikwa hivyo pale busegwe.
 
Hiyo ni kawaida sana kwa waganga wa kienyeji.
 
Bora imetokea kenya tukio lingetokea uzunguni,ingekuwa fashen huku bara la giza.
 
Tah hahahahaha.
Wagalatia nuksiiiiiii!😀😀😀:sly::sly::sly:😀
 
Kumbe wanazika na kukalisha MTU mmmmmmh makubwa wataleta mengi. Kama ni mila padri anahusika vipi

Hawa Mapadri si kama bendera tu.

We hujamuona yule padri wa Kimasai! Mwanamme kavaa shanga kiunoni ka dada marry!

Yaani ukibipu tu Mapadri wanakupigia jumla!
 
Last edited by a moderator:
Hawa Mapadri si kama bendera tu.

We hujamuona yule padri wa Kimasai! Mwanamme kavaa shanga kiunoni ka dada marry!

Yaani ukibipu tu Mapadri wanakupigia jumla!

Naona kala cha juu hapo, biashara zingine noumaaa
 
Last edited by a moderator:
Hayo wala sio ya ajabu.
Cheki hapa KONDOO wanakula majani "LIVE"!


 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom