Rais Kenyatta: Hatuwezi kuendelea na lockdown

Mbolabilika

JF-Expert Member
Jul 30, 2019
2,126
2,860
- Rais alisema serikali imeafikia uamuzi wa kuwa haiwezi kuendelea kuwafungia watu

- Alisema sasa itafikia wakati wa watu wenyewe kujilinda dhidi ya maambukizi ya coronavirus

- Nchi jirani ya Tanzania ni mojawapo wa zile ambazo hazikufunga shughuli zake za kuchapa kazi kwa ajili ya covid-19

Rais Uhuru Kenyatta ameashiria huenda 'curfew' iliyowekwa ikafunguliwa baada ya kukamilika wiki ijayo siku 21 zilizowekwa zikikamilia.

"Tumeona sisi kama serikali kuwa hatuwezi kuendelea kuwa na lockdown . . . na 'curfew'. Sasa ni lazima Wakenya warudi kwenye makazi yao na shughuli zao," Rais alisema.

Rais alisema sasa nijukumu la Wakenya kuhakikisha kuwa maambukizi ya coronavirus yanakabiliwa wakati ambapo taifa litafunguliwa.

"Sasa kwa sababu hatuwezi kuendelea na kufunga, tukifungua, halafu ugonjwa huu uendelee ujue ni wewe, na mimi na Matiang'i kuhakikisha kuwa tunalinda kila mmoja," alisema Rais.

Rais Uhuru Kenyatta alisema serikali imeafikia uamuzi wa kuwa haiwezi kuendelea kuwafungia watu.

"Nimewaeleze hawa mawaziri, haswa wa Afya kuwa Wakenya sasa wajue ni wakati wa kulindana.

Wewe ukienda kazi ni wajibu wako kulinda mama na watoto, kama serikali zile zingine kila pahali hatuwezi kuendelea kufungia watu," aliongeza Rais.

Rais alisema hayo wakati ambapo idadi ya maambukizi imefikia watu 1192 na watu 50 kufariki.

Wakenya wamekuwa kwenye kafyu ya kutokuwa nje ifikapo saa moja usiku kwa siku 28.
Kaunti tano za Nairobi, Mombasa, Kwale, Kilifi na Mandera pia zilifungiwa kwa kuwa na idadi kubwa ya maambukizi.
Mitaa ya Eastleigh Nairobi na ule wa Kale Mombasa pia ilifungwa na hakuna watu kuingia au kutoka.
 
Sasa hiyo 'curfew' na lockdown ilikuwa na kazi gani? sometimes sisi binadamu tunakuwa kama wajinga vilee..haina maana kutesa watu bure sasa hivi watu wanarudi kuchangamana kama kawa,hata kama hakuambukizwa kipindi cha 'curfew', ataambukizwa sasa.


Mnyonge mnyongeni lakini Magufuli ni genious.
 
Awaambie wale Kunguni wake wa Kibera wakatoe yale matusi mtandaoni kumtukana Magufuli bila sababu
Na Ajifunze kukurupuka Sio kuzuri
And who told you that curfews and cessation of movement was meant to be forever?. We are very greatfull for the curfew and lockdowns. It has helped in cubbing the spread of the virus to the rest of the country.
 
And who told you that curfews and cessation of movement was meant to be forever?. We are very greatfull for the curfew and lockdowns. It has helped in cubbing the spread of the virus to the rest of the country.
Hahahaha, with average of 50 new infections per day and graph is going up still you think it has helped you?.

Your minister for health said that by mid August you will have 200 infections per day, what is the rationale of lifting those useless measures at this moment?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom