Mwendapole Old
JF-Expert Member
- Dec 4, 2006
- 249
- 53
Kama unakumbuka mapambano ya Afrika kusini ili kuondoa ubaguzi. Waafrika wengi sana walikufa ikiwemo wazungu wasio na hatia. Watu waliuwawa wakiwa mashuleni na makanisani kama hawa wakenya.
Wakati yote yakiendelea, kuna watu walishauri kuwa damu inayomwagika ni muhimu kuliko mandela na kutaka waafrika wakubali tu waendelee kuishi na wazungu kama red indians walivyokubali yaishe na wakaendelea kuishi na wazungu america.
Ulichokisema hapo, hakina tofauti kabisa na wakatishaji tamaa walichosema wakati wa kupigania uhuru. Hakuna anayefurahia damu kumwagika lakini pia si kweli kusema kuwa isipomwagika basi ndio mwisho wa vifo. Madikiteta wasipoua kwa bunduki, basi wanauwa kwa starvation na magonjwa kama anavyofanya Mugabe huko Zimbabwe.
Chaguo ni je, watu wafe sasa hivi kupigania haki au wasubiri hapo baadaye watakapokufa kwa njaa na magonjwa yanayotibika?
OK. Lets shed some blood; why not start by the root cause, that is Kibaki? kwanini kila mara manyang'au yanayosababisha mauaji na migogoro huwa yanabaki hai wakati wachovu ambao ndio huwa wanawaweka madarakani wanakufa; then this time afe Kibaki!
Huu uchomaji wa nyumba za ibada na mauaji ya kiholela hayakubaliki kamwe, kibaki&co + raila&co, ni warloads wanastahili kujibu mashitaka ICC. Nashukuru EU & U.S kuingilia kati mzozo huu.
Kumuondoa Kibaki ni sawa; but at whose/what cost?
Kuondoka kwa njia ya amani,kwamba atakubali kaiba kura ajiuzulu hiyo haipo; kumuondoa kwingine ni kwa mabavu, na mabavu yanayotumika sasa sio ya kumuondoa Kibaki kama Raisi, ni ya kuondoa uhai wa wananchi wasio na hatia; ingekuwa wanamuondoa kwa njia ya bloodless coup, ambapo mwathirika angekuwa yeye mwenyewe Kibaki na wezi wenzake hapo ningekubali; as it is; kweli jamani what did the people in the church had to do with Kibaki's robbery if we call it that? hivi vifo vya walalahoi vitasaidiaje kumtoa kibaki madarakani...I mean, there are better ways of handling the matter..Kibaki kaiba kura sawa; yeye na wezi wenzie ndo washughulikiwe; hakuna mtu ataenda kwa Kibaki nyumbani au ikulu kumuuua so why the senseless killings in the street. Kwa idadi ya watu wanaokufa na kuathirika kwa mambo haya ni heri Kibaki angekufa if that would restore Kenya's peace and stability; but we can be sure kwamba hata Kibaki akiuawa leo damu ya innocent Kenyans ndo itamwagika vibaya in the name of tribalism and other stupid excuses.
Kwa maana nyingine ni kwamba kuondoka Kibaki madarakani leo kama sio kwa hiari yake basi ni kwa gharama vifo vya ya mamilioni ya wakenya; so if you are to choose a better evil you better make your calculations right
Raila alishinda uchaguzi wa urais, lakini ameshindwa kuulinda ushindi wake usiporwe. Na hata baada ya kuporwa, ameshindwa kabisa kuurejesha. Na sasa hivi ameshindwa rasmi. Kosa lake ni moja, na nililisema toka mwanzo, kuchelewa. Waswahili husema "chelewa chelewa utamkuta mwana si wako", naye kwa kosa hili, tayari "kamkosa mwana na maji ya moto"! Hiyo rally alitakiwa kuifanya siku ileile alipoapishwa Kibaki, au kesho yake na si zaidi ya hapo. Sasa hivi hamwezi tena, keshachelewa, maana amemsubiri hadi akajiimarisha upya. Sasa hivi nasikitika kusema, Raila atabakia mlalamishi tu, na kina Kibaki watakuwa wanabeza tu kelele zake wakisaidiwa na methali ya "kelele za chura hazimzuii tembo kunywa maji".
Inasikitisha, lakini imeshakuwa hivyo. Poleni sana ndugu zetu.
Mimi namshangaa sana huyu Kenyan - Tanzanian kwa kum support Raila katika njama zake za kuigawa Kenya. Kibaki anaweza kuwa mkabila lakini huyu Raila ni muuaji ana organise watu wake waenda kuua wakikuyu kanisani! jamani hata Kanisani? Hii ni hatari sana, we are carried away na hizi events zinazojiri Kenya na lakini hatari iliyopo mbele yetu ni Kenya wanaweza kumtoa mkabila Kibaki na kumuingiza muuaji Raila.
Raila kama unaona aliyekunyima urais ni Kibaki chonde chonde waache in peace wakikuyu kuendelea kulazimisha wauawe hakukusaidii, hivi utakapo ingia huko Ikulu utatawala waluo na wakalenjin tu?
Kenyan - Tanzanian naomba nikupe polite ombi pamoja na hamasa na ufurukutwa wako kwa Raila nakuhakikishia huyu mtu hana heri na Kenya, mwanzoni hata mimi nilikuwa nina sympathize nae lakini as the days goes on the man is showing his true colour hawafai wakenya na hatufai wa east africa.
All said and done si support foul alizofanya Kibaki (if any) lakini ndugu zangu wa Kenya yasije yakawakuta ya Wazambia walipomtupia virago mzee Kaunda na kumuingiza Chiluba what happened next kila mtu anajua....
Mungu Ibariki Kenya