Kenneth Kaunda atimiza miaka 93

Nimeona hizi picha nimejikuta natabasamu peke yangu, hakika hawa watu walikuwa na uchungu na Afrika kwa ujumla Allah awapunguzie adhabu za kaburi, hawakuwa waigizaji na waliwapenda kwa dhati wananchi wao
 
KK kwenye uchaguzi ule aliruhusu matokeo kurushwa moja kwa moja kutoka vituo vya kupigia kura na kutangazwa na ZBC (tbc ) hivyo kila mtu aliona mwelekeo wa matokeo (transparency ). Hakuna aliesubiri tamko la tume ya uchaguzi kujua nani mshindi. Kwa hili alionyesha njia ambayo wenzake wengi hadi leo wanakwepa. Rejea yaliyotokea kenya, Zanzibar etc kwa system ya KK tusingefika huko. BIG UP KK. Mola ampe maisha marefu kwa hili.
 
Aiseee maajabu sana Lungu naona anapeta
 
Hivi ile issue ya mwanae aitwae Kambarage Kaunda aliyeua iliishaje? Alinyongwa au kufungwa maisha?
 
Sema ndio mapenzi ya mwenyezi Mungu alimchukua Mwalimu tukiwa bado tunamuhitaji kama trafiki wa nchi,maana tangu aondoke yeye madereva hawatak kupangiwa pa kupita nadhani wote mnajua sehemu ambayo trafik hayupo madereva ufanyaje.R.I.p mwalimu happy birthday Kaunda.
 
Kila la kheri Dr Kaunda..

..mwenzio ametuacha wakiwa huku...kuna lijitu lina roho mbaya sana linafukuza kazi wasio na vyeti lkn ndugu zake linawaacha, limeacha sembe inauzwa ghali kuliko petroli hata halijali!! Lipigie hata simu tu uliambia nchi hii sio yake na watu wa kwao, ni ya watanzania wote!
 
Mungu aendelee kumuongezea miaka ya kuishi dunia.HUYU ndiye alikuwa rafiki wa kweli wa Tanzania.
 
Tunapomuongelea comredi huyu,tusisahau kukiongelea chama cha UNIP ambacho kama CCM inaelekea huko
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ