WilsonKaisary
JF-Expert Member
- Apr 4, 2017
- 392
- 951
Mungu Aendelee Kumlinda Dr KK.
Ndio faida ya kutenda mema na haki kwenye uongozi..
KK hakuwa mbadhilifu, hakuwa mvunjaji wa Katiba ovyo ovyo kama Viongozi wengi wa hivi sasa na KUBWA kupita yote alikuwa MWANA DEMOKRASIA wa ukweli.
Ndio maana kwenye Uchaguzi Mkuu wa mwisho alioshirik,i alishindwa kwenye sanduku la kura na Frederick Chiluba na kwa amani kabisa akakubali kuwa ameshindwa akakabidhi madaraka.
Hakufanya chembe ya dhuluma kwa kumpigia "Jecha" wa Zambia simu abadili matokeo na yeye ndio atangazwe mshindi japo alikuwa na uwezo huo.
Ndio maana mpaka kesho wananchi wa Zambia wanampenda na kumkubali.
Live Long Dr KK.
Viongozi wapigania Uhuru walikua na hekima sana katika kufanikisha kazi zao
Hili linanii si lina maovu mengi ndiyo maana linataka liombeweHuyu ni mmoja wa majabari ya Viongozi wa Africa wengine walikuwa ni Mwalimu Julius K Nyerere, Kwame Nkrumah, Nelson Madiba Mandela. Mungu ampe afya njema na maisha marefu. Hahitaji kupiga piga kelele huyu ili aombewe kama nanihii, matendo yake wakati alipokuwa madarakani ukiyasoma unaona kabisa alikuwa kiongozi mzuri huyu.
Huenda nae ni utamaduni wake au hushika kitambaa cheupe kuonyesha ishara ya amaniHivi ni kwa nini Kenneth Kaunda always like carry white handkerchief on his right hand?