Fyodor Dostoevsky
Senior Member
- Mar 23, 2022
- 121
- 85
Acha wivu...kwa hiyo wasisherekehe kisa elimu ni mbovu...Wanasherehekea ujinga tu. Kwa elimu gani! Hii hii ya kukariri maswali na madesa! Wakirudi nyumbani kutwa wanashinda ndani kuangalia muvi.
Kama Taifa, ni wakati sasa wa kuwa na mitaala yenye kuwaongezea zaidi wanafunzi maarifa na ujuzi, kwa ajili ya maendeleo ya kizazi cha sasa na kile cha baadaye! Badala ya hii mitaala ya sasa ambayo imeegemea zaidi kwenye kumkaririsha mwanafunzi mambo mbalimbali, huku mengine yakiwa hayana tija yoyote ile katika maisha yake.
Kwa elimu hii hii ya kukariri madesa na kusovu maswali mengi ya NECTA ndiyo nione wivu! Mtoto anafaulu mtihani, halafu anarudi mtaani akiwa hana maarifa yoyote yale kichwani!Acha wivu...kwa hiyo wasisherekehe kisa elimu ni mbovu...
Hao wazamani ambao hawakuwa wa kukariri,walivumbua nini hebu tukumbusheKwa elimu hii hii ya kukariri madesa na kusovu maswali mengi ya NECTA ndiyo nione wivu! Mtoto anafaulu mtihani, halafu anarudi mtaani akiwa hana maarifa yoyote yale kichwani!
You are not serious. Si bora hata mwanafunzi aliyehitimu mafunzo ya VETA akishangilia, kidogo nitamheshimu.
Kuna sehemu yoyote niliyosema wa zamani walivumbua kitu!Hao wazamani ambao hawakuwa wa kukariri,walivumbua nini hebu tukumbushe
Uko sahihi kabisa. Maana mtoto akitoka huko, kuna kitu anaweza kufanya ili kujiingizia kipato. Siyo hawa watoto wa Kemebos, St. Francis, St. Mary's, St. Kayumba, nkKwangu mimi mhitimu wa veta ndio mhitimu sahihi kwa hii nchi.
#MaendeleoHayanaChama
Hii elimu yetu jau sana serikali yenyewe wanajisifia kwa kujenga shule kwa hela za uviko huwa najiuliza sawa wameshajenga shule what next? Jibu ni process ile ile inajirudia kukariri tu na kurudi nyumbani kuangalia katuniUko sahihi kabisa. Maana mtoto akitoka huko, kuna kitu anaweza kufanya ili kujiingizia kipato. Siyo hawa watoto wa Kemebos, St. Francis, St. Mary's, St. Kayumba, nk
Wakitoka huko na 0, au One zao; huishia tu kula na kulala nyumbani, na pia kugombania remote sebuleni na wadada wa kazi! Huku wakisubiria kwenda hatua nyingine ya masomo, au kuhangaika na bahasha mjini wakitafuta ajira za maofisini.