Just Pray
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 2,142
- 4,779
Wajumbe wa Mkutano Mkuu Maalum wa Umoja wa Wazazi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, wamewachagua Najma Murtaza Giga (kutoka Zanzibar) na Dkt. Catherine Joakim (kutoka Tanzania Bara) kuwa wawakilishi wa Jumuiya hiyo katika nafasi za Ubunge wa Viti Maalum.
Katika uchaguzi huo, aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalum akiwakilisha Watu wenye Ulemavu, Khadija S. Taya maarufu kama Keisha, ameondolewa katika mchakato huo baada ya kushindwa kupata kura za kutosha.
Akitangaza matokeo ya uchaguzi huo, Msimamizi Mkuu ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM, John Mongela, alisema Dkt. Catherine Joakim alipata kura 561 kati ya 708, huku Najma Murtaza Giga akijizolea kura 591 kati ya 705 huku Keisha akipata kura 94 pekee kati ya kura 708 zilizopigwa.
Mongela alisisitiza kuwa uchaguzi huo umefanyika kwa kuzingatia taratibu, kanuni na miongozo ya Chama na Jumuiya ya Umoja wa Wazazi.