Kazi za Watanzania

JamboJema

JF-Expert Member
Jun 14, 2011
1,143
209
Leo katika kipindi cha Jambo - TBC wabunge wawili, wa kisarawe na mwingine, walikuwa wakiongelea kulinda ajira ya mtanzania. Walisisitiza sana 'ajira za watanzania' kutokufanywa na wageni. Swali langu ni kujua ni zipi hasa ajira za watanzania na sheria ipi inazisimamia hizi ili zisivamiwe na wageni.
 
hata kama sheria zipo au zitatungwa, za kulinda ajira za watanzania UKWELI ni kwamba, kwa serikali hii ya ccm, hakuna lolote. watu wanaapa kulinda katiba, kisha wanaghushi tena bungeni, hakuna wa kuwachukulia hatua, hivi msimamizi wa sheria kwenye hii nchi ni nani? na yeye anasimamiwa na nani? hawa Jaffo na Bulaya wanatupiga changa la macho tu, ukweli ni kwamba serikali yao ya ccm imeshindwa kusimamia sheria mchana kweupe, usimamizi wa sheria kwa nchi yetu hii chini ya ccm, ni asilimia 8%. tena pale ambapo rushwa haipo.
 
Wamunzengo kwa hiyo kwa ujumla hakuna 'specific' kazi za watanzania 'against' wageni?
 
huwezi ukaoredhesha aina za kazi halafu ukapigia mstari na kusema kuwa hizi ndo kazi za watanzania na zile za wageni. ninachokijua mimi, kuna kazi ambazo kimsingi watanzania wana utaalamu nazo na idadi ya watanzania wataalamu kwenye kazi hizo inatosheleza, kazi kama hizo inapotokea akaja mgeni halafu akazifanya ndo inazua mjadala, mf kuuza mitumba kariakoo, hivi kweli tunahitaji wachina kuja kutuuzia mitumba hapa Tanzania??? baadhi ya kazi migodini, uhasibu kwenye viwanda vinavyomilikiwa na wahindi,hivi kweli hatuna wahasibu watanzania??? na zingine za aina hiyo. cha kushangaza hata makatibu muhtasi kwenye baadhi ya makampuni hapa nchini yanaajiri watu wa nje, hii ni kukosa uzalendo na kutokuthaminiana sisi kwa sisi kama watanzania.
 
ukiangalia ma kampuni makubwa hapa nyumbani yako
chini ya wageni sasa wenyewe si watajiri yeyote wanemtaka.
 
Kwa muktadha huu basi ni kazi chache sana za wageni......Na nijuavyo wizara ya kazi ndo inatoa 'vibali vya ajira'. Inatumia vigezo vipi? Here I specifically talk about formal employments only. Wamachinga sijawaongelea.
 
ukiangalia ma kampuni makubwa hapa nyumbani yako
chini ya wageni sasa wenyewe si watajiri yeyote wanemtaka.

Hakuna sheria zinazosimamia hili.....kila mwekezaji aajiri tu atakavyo toka kokote!
 
Back
Top Bottom