Kazi ya Mungu duniani

Kazi ya Mungu duniani

BenElohimy

Senior Member
Joined
Sep 21, 2021
Posts
181
Reaction score
223
Nawasalimu wote katika jina la Yesu Kristo.

Yawezekana na wewe unayesoma mahali hapa umekuwa ukijiuliza sana ni kwa namna gani nimtumikie Mungu!!

Lakini muda huu ashukuriwe Roho Mtakatifu na Kristo wake kwa kunipa neema ya kukuandikia andiko hili.

Yohana 6:28-29 (KSW)
Basi wakamwambia, Tufanyeje ili tupate kuzitenda kazi za Mungu?

Yesu akajibu, akawaambia, hii ndiyo kazi ya Mungu, mmwamini yeye aliyetumwa na yeye.

Unaona baadhi ya watu waliwahi kumuuliza wafanyeje ili wazitende kazi za Mungu, cha kushangaza Yesu anawajibu tena kwa kuwasahihisha, kwamba hakuna kazi za Mungu bali kuna kazi ya Mungu ambayo ni kumwamini Yeye aliyetumwa na yeye.

Akiwa na maana ya kwamba kazi kubwa unayotakiwa kuifanya ni kumwamini Yesu Kristo aliyetumwa na Mungu BABA.

Kutoa mapepo na mengine kama haya siyo kazi ya Mungu ni matokeo yanayotokana na kazi ya Mungu.

Basi wewe uliyepata neema ya kusoma andiko hili na kama una imani basi waambie watu habaari za Mungu kuliko za wanadamu.

Kama hauna Mungu basi unaye shetani.
 
Ngoja niendelee kupiga stori na shetani
Nalog off  Z
 
Sawa,

Niambie nani alijenga hekalu la pili kule Yerusalemu.

Je, hekalu la tatu litafanikiwa kujengwa?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom