Phillipo Bukililo
JF-Expert Member
- Dec 29, 2015
- 18,487
- 13,612
Katika hotuba mojawapo ya Mwalimu Nyerere, anasikika akiongelea idadi ya wataalam aliokuwa nao wakati nchi ikianza safari ya kuwa huru mwaka 1961.
Desemba mwaka huu imetimia miaka 55 tangu safari hiyo ianze. Ukizitazama picha za mitaa ya Dar, Arusha na Mwanza ambazo zilipigwa siku za mwanzoni za Tanganyika huru halafu ukazilinganisha na hizi za sasa, tofauti ni kubwa sana.
Mengi mema na mabaya yamefanyika ndani ya uongozi wa awamu zote tano tangu uhuru. Mpaka tumefikia hii awamu ya tano, kujifunza na kukosea kumekuwa ndio utaratibu wa maisha binafsi na yale ya kiuongozi.
Wakati mwaka wa kwanza wa awamu ya tano ukiwa umemalizika, yapo mema yenye kustahili kupewa nafasi kubwa na muhimu na mabaya pia.
Lakini hii ni Tanzania ambayo walioelimika na wanaoendelea kuelimika ni wengi sana. Uwezo wa watu kuhoji na kujenga hoja, ni mkubwa sana.
Hivyo kazi ya kuelezea kwa ufasaha malengo ya mipango ya serikali ya muda mfupi na mrefu, isifanyike kwa kuongozwa na kile kiburi cha madaraka. Bali ifanyike kwa weledi mkubwa kwani anayeelezewa mipango hiyo, anapoweza kushawishika katika kuikubali ndipo baraka zake zinapoweza kufanikisha malengo ya serikali.
Ikiwa wakati wa uhuru madaktari hawakuzidi watano, leo hii tunao wengi sana, unapojenga hoja kama mtu wa serikali basi ujue upana wa hadhira inayoupokea ujumbe wako kwa wakati mmoja.
Unapoelezea mipango ya wizara kwa mfano wa sheria, ujue kwamba kuna wanasheria wengi tu wanaoandaliwa vyuoni na wengine wapo kazini, basi na ujenge hoja huku ukitambua mrejesho utakaoupata kutoka kwa wadau wengi wa sekta ya sheria.
Afrika imekuwa na tatizo la wenye kutakiwa kuelezea wakifanyacho kwa niaba ya wananchi, kushindwa kuwashawishi watu wengi juu ya kile wakifanyacho.
Mwaka 2017 na uwe ni mwaka ambao mipango na mikakati ya kiserikali itakawasilishwa kwa wananchi, katika namna ambazo zitaendana na wingi wa watu wenye weledi katika sekta fulani.
Kazi isiishie katika kuwasilisha ripoti fulani bali muwasilishaji atambue umuhimu wa weledi katika uwasilishaji wake ili apunguze manung'uniko ya walengwa na wasio walengwa wa kile alichokiwasilisha.
Mungu atuongoze wana Jamii Forum ili tuumalize mwaka 2016 kwa amani na tuuanze mwaka 2017 kwa matarajio chanya katika maisha yetu.
Mungu atubariki sote.