Kazi tumewapa mafisadi, tulitegemea nini?

Kazi tumewapa mafisadi, tulitegemea nini?

G Sam

JF-Expert Member
Joined
Apr 20, 2013
Posts
12,282
Reaction score
38,876
Miaka kadhaa iliyopita Andrew Chenge akiwa uwanja wa ndege wa JNIA baada ya kutimuliwa kutoka kwenye Ziara ya Kikwete huko ughaibuni kutakakopigwa kura ya katiba, aliwaambia waandishi wa habari kuwa bilioni kwake ni vijisenti tu huku akionyesha kiburi na dharau kubwa.
"Hii bilioni kwangu ni vijisenti tuu, hii inaonyesha ni jinsi gani nina jeuri kuliko Watanzania wengine, hivi ni vijisenti tu"

Hayo yalikuwa maneno yaliyotamkwa na huyu bilionea mpya mwanasiasa aliyejulikana enzi hizo huku akiwa hana biashara ya kumuingizia fedha nyingi inayotambuliak!

Baadaye kidogo bilionea Chenge akiwa anaendesha gari akamgonga dereva wa bajaji maeneo ya Mwenge.Alipekekwa mahakamani na hukumu ikatoka ambapo Chenge alipigwa faini isiyozidi laki tatu za kitanzania! alipotoka viunga vya mahakma huku akitanua mikono aliwaambaia waandishi wa habari huku akionyesha dharau na kiburi "nipigeni picha, mimi ndiye rais wa Tanzania, rais wenu"

Baada ya hapo Chenge akaanza kuandamwa na Samuel Sitta akimuita fisadi asiyetakiwa ndani ya CCM.

Majuzi Chenge akataka kuwania uwenyekiti wa BMK akipambana na Sitta aliyekuwa akimtuhumu huyu Chenge kuwa ni fisadi wa mali ya umma! Baadaye Chenge akajitoa na kumuachia Sitta aendelee (hapa ndiyo nataka nipagusie)

Kujitoa kwa Chenge kwenye kinyang'anyiro cha uwenyekiti wa BMK hakukuwa hivihivi, Sitta ni mtu wa mipango sana hasa pale anapotaka madaraka, yuko tayari kufanya lolote (rejea kwa yaliyotokea huko nyuma).Hapa Sitta alipanga kumpa Chenge mamlaka ya kuandika katiba huku akimuahidi posho ya laki tano kwa siku fedha za Kitanzania. Chenge udhaifu unajulikana, hapo hana ubishi!

Tunachokiona hapa ni jinsi viongozi wengi wa CCM walivyo mafisadi wa kutisha! wanaposalitiana hapo ndo uvumilivu huisha na kuishia kubwatukiana kama afanyavyo Sitta!
Hawa ndiyo watu waliowekwa mstari wa mbele kuongoza katiba, kuiandika na haohao ndiyo viongozi wa maadili ya utumishi wa umma!

Pengine hawa CCM wana neno tofauti lenye "tafsiri ya maadili" tofauti na sisi tunavyofikiri!
Niliwaambia na leo nawaambia tena kuwa CCM
kupitisha rasimu ya Warioba ni sawa na kujivua nguo! Hawako tayari kubaki uchi waonekane!

Walipomzomea Warioba siku ya kuipeleka rasimu bungeni, hapo wakina sisi tilishajua kilichopangwa, kinachofuata na kitakacho tokea! Ukweli umeonekana kwa wote!
 
Back
Top Bottom