Ninashindwa kupata maneno mazuri ya kutumia ili kumaanisha majonzi, kilio na masikitiko yangu. Kwa kweli inaudhi, inakera na inaumiza.
Kwamba kwa miaka kadhaa sasa nilitafuta namna ya kukabiriana na ugumu wa maisha kwa kujihusisha na kilimo. Siyo siri, mwanzoni niliona nuru ya mafanikio japo kwa mbali ikijongea. Hii ilinipa hamasa ya kuimarisha zaidi shughuli zangu na hivyo kuanza kukubaliana na kauli kwamba kama mnataka mali mtayapata shambani.
Sijui ni laana gani iliyotukumba gahafla, huenda ni kweli kwamba Watanzania tulio wengi tuna ngekewa ya umaskini. Hivyo kila jitihada yetu lazima ikumbane na vikwazo tena vya kutengeneza ama kulazimiahiwa.
Ghafla soko letu likafungwa na hivyo kutulazimisha kupata hasara. Ajabu na kweli gunia la mahindi ni 20,000 - 30,000! Halafu kuna watu eti wameajiriwa kushughulikia changamoto zetu. Kwa msingi huu ninaamini sitakosea nikisema tu wajinga wa kutupwa. Haiingii akilini watu na vyeo vyao wanajua gharama za uzalishaji lakini ndio wanaolazimisha tuuze kwa bei za kijinga.
Inaumiza sana, lakini kwa kuwa sisi ni wanyonge hatuna la kuwafanya. Na kodi tutawapa ili mle mpate nguvu za kutoa matamko ya kijinga yanayotuumiza sisi walalahoi.
Sent using Jamii Forums mobile app