Kazi Na Uwajibikaji

Dec 16, 2015
21
1
Mtazania mdau wa jamii forum ifahamike kwamba tangu mwanzo wa utawala awamu ya tano uanze chini ya usimamizi wa Mh.Dr.John Pombe Maghufuli kwa namna moja au nyingine moto wake unatia moyo.
Katika Utendaji Wa Kisiasa Na Kijamii Viongozi Wa Ngazi Mbalimbali Walijisahau Sana Hasa Katika Kutimiza Wajibu Wao.
Tumeshuhudia mabadiliko tofauti yakiwemo ya watu kufukuzwa kazi na wengine kusimamishwa kwa uchunguzi zaidi.Hii ni dalili nzuri ya kwamba serikali ya awamu ya tano inatia moyo hasa kwa wapiga kura wake ukilinganisha na awamu ya Mh.Dr.Jakaya Kikwete.Kwa Jambo Hili Tutakuwa Wachoyo Wa Fadhila Kama Hatutawapongeza Watumishi Wa Serikali Moja Kwa Kuhimili Kishindo Cha Maghufuli Na Pili Kwa Uwajibikaji Wa Lazima.
Ndugu Watanzania Wenzangu Kufanya Kazi Ni Wajibu Na Wajibu Huu Ni Wa Kila Mtanzania.
Tusisubiri Ziara Za Kushitukiza Za Watendaji Wa Mawaziri Na Rais Uje Kuhimiza Ufanyaji Wa Kazi.
Tuamke Watanzania Kuleta Maendeleo Ya Nchi Yetu Tanzania.Kwa Waalimu,wabunge,mawaziri,na Watu Wote Waserikali Hii
TUWAJIBIKE.
 
Back
Top Bottom