Kazi mshanara mkuuubwa barrick gold!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

Mpeni sifa Yesu

JF-Expert Member
May 23, 2010
646
129
TAFADHALI samahani kwa wale waliofungua wakifikiri ni kazi. Kuna kundi la watu wametangaza kuwa wao ni Barrick Tanzania na wakatangaza nafasi za kazi nyingi sana mkoani shinyanga kule KAHAMA etc. watz wengi waliapply inavyosemekana na wamekuwa kwenye mawasiliano nao mara kwa mara. kutokana na hilo, ili wapate kazi kuna jobless wengi wametakiwa kulipa wengine 500,000/= wengine millioni etc na inasemekana wametoa pesa hizo. kuna kikundi cha wana usalama tunashirikiana nao shinyanga kwaajili ya suala hilo tu special, tunaomba yafuatayo kwa wote ambao wamedhurumiwa.
  1. JAMBO LA KWANZA, kama umedhulumiwa kwa namna hii, tafadhali tunaomba uwasiliane namimi bila kuchelewa ili niwasilishe majina ya watu hao polisi.
  2. kama unazo namba za simu ambazo labda umekuwa ukiwatumia pesa kwa njia ya mpesa etc, utuletee namba hizo kama ushahidi nami nitawasilisha kwa wanausalama.
  3. kama umedhulumiwa na unao ushahidi wa kutosha either kwa njia ya simu uliyowasiliana nao na pengine mlishaonana uso kwa uso, wasiliana nami au fika kituo chochote cha polisi watasaidia kuwasiliana nasi, na mimi nitafoward suala lako kwa wahusika.
  4. wasiliana nami kwa kupitia email mpani.sifa.yesu@gmail.com, bila kuchelewa.
Nashukuru kwa ushirikiano. si vyema sana kuandika hii kitu hapa, lakini kwasababu imewatokea wengi, na kwenye kampuni yetu ya barrick kumekuwa na matukio mengi ya namna hii, nimeona ni vyema kuiweka hapa ili kama kuna watu wengine wanaotafuta kazi wajue mitego ya hawa watu wabaya. pale wewe unapohangaika kutafuta kazi, wenzio wanahangaina namna gani watakupiga..pengine hela zenyewe umezikopa tu, na una matumaini...naomba tushirikiane kwa hili na mengine, na NINAAMINI JF ITAKUWA KITUO KIZURI CHA MATANGAZO YA WALE WALIOIBIWA, au mtaunda kitu fulani cha ku tackle issue za kuzuia uhalifu wa namna hii. Asanteni sana., na Mungu awabariki.
 
Aisee mbona ni hatari sana. Jamani tuwe makini sana na matapeli wa namna hii.
 
Nilitaka kuingia kwenye mkenge huu nikashtuka mapema ila nikawaambia mie hela ntawapa ila ni apale nitakaposaini barua ya ajira na hela yangu mkononi nawapa zote hata kama laki saba wakachikichia sijawaona tena tusio na ajira tunaliwa sana.
 
TAFADHALI samahani kwa wale waliofungua wakifikiri ni kazi. Kuna kundi la watu wametangaza kuwa wao ni Barrick Tanzania na wakatangaza nafasi za kazi nyingi sana mkoani shinyanga kule KAHAMA etc. watz wengi waliapply inavyosemekana na wamekuwa kwenye mawasiliano nao mara kwa mara. kutokana na hilo, ili wapate kazi kuna jobless wengi wametakiwa kulipa wengine 500,000/= wengine millioni etc na inasemekana wametoa pesa hizo. kuna kikundi cha wana usalama tunashirikiana nao shinyanga kwaajili ya suala hilo tu special, tunaomba yafuatayo kwa wote ambao wamedhurumiwa.
  1. JAMBO LA KWANZA, kama umedhulumiwa kwa namna hii, tafadhali tunaomba uwasiliane namimi bila kuchelewa ili niwasilishe majina ya watu hao polisi.
  2. kama unazo namba za simu ambazo labda umekuwa ukiwatumia pesa kwa njia ya mpesa etc, utuletee namba hizo kama ushahidi nami nitawasilisha kwa wanausalama.
  3. kama umedhulumiwa na unao ushahidi wa kutosha either kwa njia ya simu uliyowasiliana nao na pengine mlishaonana uso kwa uso, wasiliana nami au fika kituo chochote cha polisi watasaidia kuwasiliana nasi, na mimi nitafoward suala lako kwa wahusika.
  4. wasiliana nami kwa kupitia email mpani.sifa.yesu@gmail.com, bila kuchelewa.
Nashukuru kwa ushirikiano. si vyema sana kuandika hii kitu hapa, lakini kwasababu imewatokea wengi, na kwenye kampuni yetu ya barrick kumekuwa na matukio mengi ya namna hii, nimeona ni vyema kuiweka hapa ili kama kuna watu wengine wanaotafuta kazi wajue mitego ya hawa watu wabaya. pale wewe unapohangaika kutafuta kazi, wenzio wanahangaina namna gani watakupiga..pengine hela zenyewe umezikopa tu, na una matumaini...naomba tushirikiane kwa hili na mengine, na NINAAMINI JF ITAKUWA KITUO KIZURI CHA MATANGAZO YA WALE WALIOIBIWA, au mtaunda kitu fulani cha ku tackle issue za kuzuia uhalifu wa namna hii. Asanteni sana., na Mungu awabariki.

Inaonekana wew ni mtu wa ndani ya Barrick kwa jinsi ulivyoandiaka, ila napata mashaka kwa nini hukutoa official Email (Outlook/Webmail), na umetunia email ya kawaida ambayo hata mimi na huyu anaesoma anaweza kua nayo? Au unataka kujua nia wangapi washatapeliwa ili kuwalinda matapeli hao....?

MTAZAMO TU MSIJENGE CHUKI.
 
inaonekana wew ni mtu wa ndani ya barrick kwa jinsi ulivyoandiaka, ila napata mashaka kwa nini hukutoa official email (outlook/webmail), na umetunia email ya kawaida ambayo hata mimi na huyu anaesoma anaweza kua nayo? Au unataka kujua nia wangapi washatapeliwa ili kuwalinda matapeli hao....?

Mtazamo tu msijenge chuki.

hata na majani!
 
Inaonekana wew ni mtu wa ndani ya Barrick kwa jinsi ulivyoandiaka, ila napata mashaka kwa nini hukutoa official Email (Outlook/Webmail), na umetunia email ya kawaida ambayo hata mimi na huyu anaesoma anaweza kua nayo? Au unataka kujua nia wangapi washatapeliwa ili kuwalinda matapeli hao....?

MTAZAMO TU MSIJENGE CHUKI.
kama mimi ni mtu wa ndani ya barrick au la, hilo si la muhimu, cha muhimu ni kwamba, kuna watu wamepigwa mamilioni mengi sana, na hadi hivi sasa kuna wengine wameshakamatwa, mtawasikia kwenye vyombo vya habari muda si mrefu ndani ya mwezi huu wa saba wakia court. it is not necessary kwamba utumie email yangu, kwasababu mimi sijaandika kwaniaba ya office, hata hivyo, waliopiga sio wafanyakazi wa barrick, bali ni watu wanaojifanya wafanyakazi wa barrick kumbe siyo. kuweni makini ndugu zangu.
 
ukiona mwenzio ananyolewa, tia maji kibichwa chako, chezesha akili kabla hujaliwa.
 
Nina wasiwasi na wewe mwandishi kwanza taja hizo nafasi za kazi watu walizohonga ili wapatiwe.Kama ni professional job watu hawawezi kudanganywa maan mtu habembelezi na anajiamini na huwezi kumshawishiwa kutoa hongo.Isije ikawa ni zile kazi zenu za ma miner mnawadanganya wasoteaji wa hapo Kahama na Kakola mnawalia pesa zao na kazi zenyewe ni za undeground.Sasa hii topiki umeileta hapa si pake maana miner hana muda wa kuangalia mtandao yeye muda wote yuko underground anachimba madini.
 
It might b true! mliopigwa polen jaman. Tuwe makn jaman ktk utafutaji wa kazi. Siyo matangazo yote ni ya kweli.
 
Back
Top Bottom