MAHANJU
JF-Expert Member
- Aug 26, 2014
- 5,252
- 8,003
Kwa mujibu wa katiba ya JMT ni kwamba mbunge anaweza kua mtu yeyote anayejua kusoma na kuandika tu!
Sasa mbunge anayejua kusoma na kuandika ndio atunge Sheria ikatafsiriwe na Mahakama? Yaani kuna mambo yanatia hasira kweli katika nchi hii! Mbunge anayejua kuandika jina lake na kulisoma atunge sheria ikatafsiriwe na Majaji au mawakili waliomaliza school of low? Mtu ukitafakari sana haya inafika mahali unajutia kuzaliwa katika taifa hili!
Kwa hali hii naweza kusema kua tunao wabunge wachache sana wanafanya kazi ya kutunga sheria ila mamia ya wabunge hii kazi hawawezi, na wameenda wakiwa wanajua kabisa kua kazi mama ya bunge ni kutunga sheria.
Ifike mahali mgombea asiyekua na elimu tuachane naye kabisa hata kama katiba inaruhusu. Tutumie uhalisia uliopo kulinusuru taifa letu ingawa kuna wachache hawayataki kabisa mabadiliko ya katiba kwa manufaa yao.