Kazi Barrik

Mchaga

JF-Expert Member
Apr 11, 2008
1,378
202
Wakuu ni mara ya pili sasa najaribu kuomba kazi kupitia email ya Barrik lakini kila nikituma email inarudi na error sasa naanza kupata wasiwasi kuwa wanachokifanya isijekuwa ni kiini macho cha kutangaza tu, naamini kuna watu wa Barrik wanaweza kusaidia hii.

Mfano leo nimetuma CV nimerudishiwa na meseji ifuatayo:

----- The following addresses had permanent fatal errors -----
<recruitment@africanbarrickgold.com>
(reason: 550 No such user - psmtp)
<recruitment@barrick.com>
(reason: 550 No such user - psmtp)
 
Tangazo la kazi halikuonyesha namba zao za simu?

Jaribu kuwatwangia simu na utapata jibu la uhakika na haraka zaidi
 
no, labda kuna tatizo la netwek huko kwao. miaka ya nyuma niliomba kazi nikwawa najibiwa hivyohivyo ila baadaye nilijibiwa nikaenda kwenye interview. tulishindana kwenye salary. keep applying dude!!
 
nadhani labda ni mambo ya network hayo, nadhani hao jamaa wanaunganishwa na jamaa wa south africa kwenye head quarter yao
 
usikate tamaaa ila jaribu tu...maana network ya barrick huwa inawasumbua sumbua mara kwa mara!
 
hv na nyny mnaamin kampun kubwa kama ile email address inawazingua je website yao au simu zao cndo kabisa sema kwamba wamechachukuwa wa2 walio watosha wameamua kuzma au kublock email mana wameshapokea email za kutosha bac imekula kwako uliechelewa inawezekana wanablock server 2 kwisha so try next time wanapotangaza kaka HII NDO TANZANIA
 
Jaribu hi ya buzwagi buzrecruitment@barrick.com ukipata au kuko toa feedback please.

Tumia recruitment@barrick.com hii ni sawa na recruitment@africanbarrickgold.com na hizi ni e-mail addresses za Barrick Bulyanhulu - Kahama. Hiyo ya buz..... iache hawahusiki na kazi iliyotangazwa na uongozi wao uko tofauti pia japo uko similar.
Kesi ya nyani unampelekea ngedele?

Pole!
Do not give up.

Mi niliapply jioni kwenye saa kumi na moja kesho yake saa tano asubuhi nikapigiwa simu kuitwa kazini - siyo kwenye interview (vyeti walikuja kuniomba nikiwa kazini tayari kwa ajili ya kumbukumbu). Kwa sasa sipo huko nipo sehemu nyingine (sisemi kwamba BARRICK ni wabaya, NO! Ni wazuri sana tu lkn sehemu niliyopo iko juu kuliko Barrick)
 
hv na nyny mnaamin kampun kubwa kama ile email address inawazingua je website yao au simu zao cndo kabisa sema kwamba wamechachukuwa wa2 walio watosha wameamua kuzma au kublock email mana wameshapokea email za kutosha bac imekula kwako uliechelewa inawezekana wanablock server 2 kwisha so try next time wanapotangaza kaka HII NDO TANZANIA

Si kweli, usiwakatishe tamaa wenzako bana. Msj delivery huwa zinafail hata microsoft, ijekuwa barrik!!!!
 
Bora umesema. Kila mtu ninayemjua aliyeomba barrick wamepata email ya failure hata kabla ya deadline.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom