Kaya 3,255 kunufaika na Majiko ya Gesi Katavi

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
1,446
Reaction score
2,093
Wananchi Kijiji cha Usevya Wilaya ya Mlele mkoani Katavi wamepongeza hatua zinazochukuliwa na Serikali kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) katika kuhakikisha wanafikiwa na nishati safi ya kupikia kwa bei ya ruzuku.

Wametoa pongezi hizo kijijini hapo Agosti 12, 2025 wakati wa zoezi la usambazaji wa majiko ya gesi (LPG) ya kilo sita na vichomeo vyake kwa bei ya ruzuku ya shilingi 19,500 kwa kila jiko.

"Tunaishukuru Serikali kwa kutuletea majiko haya yanakwenda kurahisisha maisha yetu, majiko haya pia ni mkombozi wa mazingira naamini ukataji wa miti unakwenda kupungua,” alisema Davis Majaliwa Mkazi wa Usevya

Kwa upande wake Christina Sindano mkazi wa Kijiji cha Usevya alimshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwa mstari wa mbele katika kampeni hiyo ambayo alisema inanufaisha wananchi wake hususan kina mama

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kijiji cha Usevya, Focus Kapongwa alisema wananchi kijijini hapo wamekuwa na mazoea ya kukata miti kwa ajili ya kuni na mkaa lakini kufika kwa mradi kutapunguza ukataji holela wa miti.

Akizungumza kuhusu mradi, Mtaalam wa Jinsia na Nishati wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Dkt. Joseph Sambali alisema mradi huo kwa Mkoa wa Katavi unatekelezwa kwa kushirikiana na Kampuni ya Taifa Gas Limited ambapo jumla ya majiko 3,255 ya gesi (LPG) ya kilo sita yakiwa na mafiga na viwashio vyake yatasambazwa katika kila Wilaya ya Mkoa wa Katavi kwa bei ya ruzuku

Kwa upande wake Katibu Tawala Wilaya ya Mlele, Yahaya Mbulu alitoa wito kwa wananchi kuchangamkia fursa zinazotolewa na Serikali ikiwemo ya nishati safi ya kupikia ili kulinda afya zao na kuhifadhi mazingira

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…