Kausikilize huu wimbo upate madini ya mtaani.

Kausikilize huu wimbo upate madini ya mtaani.

Strong boy

Member
Joined
May 31, 2019
Posts
7
Reaction score
5
MUZIKI NA UCHAMBUZI


Wimbo: Kesho yetu
Msanii: one the incredible
Albamu: Soga za mzawa
Mtayarishaji: texas
Studio: mlab ( tamaduni music)


Muziki unaowakilisha utamaduni wa hip hop , umekuwa ni muziki unaopendwa duniani kutokana na vitu ambavyo vimekuwa vikizungumziwa na aina hii ya muziki.

Katika sehemu hii tutaichambua moja ya kati ngoma kali za hip hop inayokwenda kwa jina la kesho yetu.
Ngoma hii imeandikwa na one the incredible na kuchanwa na yeye mwenyewe akimshirikisha Songa. Imefanyika mlab chini ya tamaduni music mtayarishaji akiwa texas

One the incredible a.k.a moko wa miujiza ni miongoni mwa wasanii wakali wa hip hop hapa tz. Ngoma zake nyingi zenye tungo za kufikirisha zimekuwa zikifanya vizuri sana mtaani ambako amejijengea heshima kubwa.

Katika ngoma ya kesho yetu , one amejitahidi sana kuelezea jinsi gani watu wengi hasa vijana ambavyo wamekuwa na mashaka juu ya future ya maisha.
Katika ngoma hii , One amejitahidi sana kuelezea uhalisia wa maisha ya mtaa.

Katika verse ya kwanza, one anaanza kwa kuongea na Muumba wake amjalie nguvu na ujasiri pale anaposema " mwenyezi nijalie nguvu na roho ya ujasiri/ ili nami niweze amini kesho bora ya utabiri". hapa unaweza kuona jinsi gani one, anaonesha umuhimu wa kumtanguliza Mungu katika kila jambo.

One anazungumza pia na wazazi , kwanza anaanza kwa kumuuliza mama yake maswali mbalimbali ambayo hakupata majibu. One anauliza kwanini ng'ombe wa maskini hazai? Alafu kwanini duke (ambaye ni mtayarishaji wa muziki) akienda ofisini havai tai? Yaani anaenda kisela tu. Inawezekana one alikaririshwa kama tulivyokaririshwa wengi kuwa kwenda ofisini kuna aina yake ya mavazi.

Lakini pia One anashangaa , kwanini mtoto wa jirani asubuhi amimini chai (hapati kifungua kinywa). Hii pia inaonesha jinsi gani watu wengi tumekariri kwamba asubuhi chai lakini nikuambie tu kuna familia nyingi ambazo kwao chai ni ndoto.

Katika verse hii ya kwanza, One anakumbusha ahadi ambazo alipewa na Baba yake pale anaposema "Baba alisema atamuozesha shangazi/Dada atapata mkopo ,kaka atapata kazi." ukiziangalia ahadi zote hizi, ni matumaini ya familia nyingi za maisha duni. Hapo anaonesha jinsi gani kuolewa, mkopo na ajira ni mategemeo ya vijana wengi wa mtaa.

Verse ya pili one anaanza kutupa tafsri ya maisha na changamoto zake, pia hakuacha kuitupia lawama serikali kwa jinsi inavyoongoza nchi. One anasema "Haya maisha ni safari, ila hili gari ni bovu/ hii hali hatari, serikali ina uovu"

One pia ametumia verse ya pili kuongea na mzazi (Baba) juu ya mambo mbalimbali. Anamkumbusha Baba juu ya kusali, juu ya kusomesha watoto. Anamkumbusha kuwa yeye(One) ni taifa la kesho. Anamkumbusha Baba yake juu ya kutunza heshima yake na kumtunza na kumjali mke wake. One anasema "Baba sali sana, muumba akupe mema/ acha hali ya kujuana kayumba asome tena". pia anasema "mzazi mjali mkeo sio kimeo/ kesho itafika vipi, hili taifa likifa leo?

verse ya tatu One anagusia changamoto za elimu, ukosefu wa madawati , walimu, vifaa vya kufundishia na kujifunzia na usafiri ni changamoto kubwa za elimu. One anasema "watoto wataipendaje elimu na shule wanakaa cchini?/ usafiri sio bure hata kama unakaa mjini"

one pia anawaasa vijana juu ya mahusiano ya kimaoenzi na kujikinga na ukimwi , One anasema " Hili swali ni kwa kijana kama mimi/unajikinga vipi na sura nzuri zimevaa ukimwi?" anaendelea "unashangaa nini? Biashara hazitembezwi/jichunge sana mwanamke imara hajilengeshi na hawalegezi".

one pia anawatia moyo vijana kwa kuwaambia wakijituma watatoboa , anasema "maisha bora hayako mbali tatizo hatujui kulenga / tumemfanya dhiki rafiki hatujui kumtenga"
Strong boy
#pundachizi
MUZIKI NA UCHAMBUZI
 
Bonge la kichupa uno katisha hajawahi niangusha, bila kusahau na muvi yao kutoka bongo hoodz imeachiwa siku si nyingi
 
Samahani hivi Ajaimba na Nikki mbishi


"hadithi za mitaa huponya kama dawa"
 
Ngoma kali mno. Sitiari,tashbiha,tabaini,mjalizo,tashtiti na kila aina ya tamathali za semi zimeundwa vyema na bwana Moja(Uno) [emoji91]
 
Samahani hivi Ajaimba na Nikki mbishi


"hadithi za mitaa huponya kama dawa"
Hapana kaka, hiyo unayo iongelea wewe inaitwa soga za mzawa ambayo pia ndio jina la albamu. Ambapo katika hiyo hiyo albamu kuna wimbo unaitwa kesho yetu amemshirikisha songa , ndiyo wimbo niliouzungumzia kwenye uzi huu. Asante.
 
Ngoma kali mno. Sitiari,tashbiha,tabaini,mjalizo,tashtiti na kila aina ya tamathali za semi zimeundwa vyema na bwana Moja(Uno) [emoji91]
Bila kusahau ujumbe uliofikishwa vizuri kwa hadhira. Binafsi ni moja ya ngoma za hip hop ninazozikubali sana.
 
Hapana kaka, hiyo unayo iongelea wewe inaitwa soga za mzawa ambayo pia ndio jina la albamu. Ambapo katika hiyo hiyo albamu kuna wimbo unaitwa kesho yetu amemshirikisha songa , ndiyo wimbo niliouzungumzia kwenye uzi huu. Asante.
ha ha ha kumbe "kesho yetu"
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom