sangujoseph
Senior Member
- Nov 30, 2015
- 164
- 183
By Sangu J
Kuanzia Februari 2 nakutana na mawazo mbalimbali kutoka kwa watu wangu wa karibu wakinihusia umekuwa ukitoa maoni mbalimbali kwenye mijadala ya Kitaifa lakini mbona hatuoni ukitoa maoni yako Juu ya kauli zinazotolewa na baadhi ya viongozi wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana ya UVCCM dhidi ya Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe.
Kwanza nikiri ni kweli nimeziona kauli zilizotolewa na vijana wenzangu akiwemo Waziri Mkuu wangu wa zamani wakati nasoma Chuo cha Tumaini Iringa ndugu Kenani Kihongosi kwamba watu wanaosaliti nchi sharti 'wauawe', kwa tafsiri ya wengi ni kwamba wameelewa Ndugu Zitto anapaswa kuchukuliwa hatua kwa alichokifanya.
Kwanza mimi siamini kama Ile kauli ni msimamo wa Jumuiya wa umoja Vijana Kwa sababu umeundwa kwa mujibu wa Sheria na taratibu za nchi yetu ambazo zinaitaka kulinda misingi ya Amani na afya ya nchi na kuheshimu Haki ya mtu mwingine kuishi, Kwa hiyo naungana na Mwenyekiti wangu Ndugu Kheri James ambaye kupitia Mwananchi (Mwenyekiti UVCCM afafanua kauli yake, ampinga aliyetaka) ameeleza vizuri kuwa alichosema Ndugu Kihongosi si msimamo wa Jumuiya hiyo.
Mimi binafsi Kwa mapenzi na nchi yangu naheshimu Haki ya kuishi ya kila kiumbe ambacho kipo Tanzania as long as ni kipo kwenye ardhi ya Tanzania basi kinapaswa kisivunjiwe Haki yake ya kuishi.
Lakini mjadala kauli za Viongozi wa Jumuiya (UVCCM) nadhani haujaja from no where umekuja baada ya Zitto kuandika Barua kwenda WB akishinikiza Tanzania kutopatiwa mkopo wa zaidi ya Dola Mil. 500 kutokana na sababu alizoieleza yeye kwamba mkopo huo hautawafikia walengwa.
Ukisikiliza hoja za Zitto kwenye mahojiano yake na Zuhura Yunus wa BBC inaonesha dhahiri kuwa hofu ya Zitto ni huenda mkopo huo ungetumika kisiasa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2020.
Sababu nyingine anayoieleza Zitto ni kuwa tusipewe mkopo kwa sababu pia Sera yetu ya elimu ni Baguzi Kwa kutoruhusu watoto wanaopata ujauzito kuendelea kimasomo na wanafunzi ambao hawana ujauzito au kujihusisha kimapenzi kabisa lakini Serikali ilishaeleza wazi kuwa lengo la kumtoa mwanafunzi aliyepata mimba kwenye mfumo wa kawaida na kumpeleka kwenye mifumo mingine kwanza ni kumuondolea kuonekana si mtu wa kawaida kwenye Jumuiya ambayo haikumzoea kwenye hali ya mimba na huenda ingemfanya atengwe zaidi.
Japo wanasema mimba si ulemavu, kwanini kuna madarasa ya maalum ya watu wenye ulemavu na, je wanabaguliwa? HAPANA. Ila kutokana hali yao si vyema sana kuwaunganisha na wanafunzi wengine kwa sababu ikawafanya kuwa wanyonge zaidi.
Kiukweli mimi binafsi siungi mkono hatua ya Zitto kushinikiza Tanzania isipatiwe mkopo ambapo asilimia 70 ya sababu zake hazihusiani na masuala ya elimu bali ni za kisiasa.
Comrade Sangu J
0712861292
Sent using Jamii Forums mobile app