Mwanahabari Huru
JF-Expert Member
- Mar 9, 2015
- 14,242
- 34,917
Kauli aliyoitoa Mheshimiwa Rais John Magufuli tarehe 1 Mei 2017, akiwahutubia wafanyakazi Mjini Moshi na kunukuliwa na vyombo vya habari kuwa; “kuhusu kuongeza mishahara, mwaka ujao wa fedha 2017/18, Serikali itapandisha mishahara ya wafanyakazi wote,itapandisha madaraja yao na pia nyongeza zao za mishahara watapewa”.
Kwa masikitiko makubwa Mwaka huu tarehe 1 Mei, 2018 Kauli iliyotolewa na Mheshimiwa Rais John Pombe Magufuli kwamba, hana mpango wa kupandisha mishahara ya watumishi wa umma hadi atakapomaliza kutekeleza miradi mikubwa ya Stigler’s Gorge, Reli kwa kiwango cha “standard Gauge” na ununuzi wa ndege pamoja na ukarabati wa viwanja vya ndege ni uamuzi wa kisikitisha sana na kinyume cha ahadi yake alyoitoa Mwezi Mei 2017.
Miradi hii mikubwa ni ya muda mrefu na watumishi wa umma wataendelea kuwa na maisha magumu kwa sababu mishahara yao haikidhi mahitaji muhimu ya kuendesha familia zao.
Mishahara ya watumishi haijapandishwa kwa takriban miaka minne sasa. Ongezeko la kila mwaka (annual increament) kutegemeana na muundo wa utumishi uliotekelezwa Novemba 2017, ni ongezeko dogo sana ikilinganishwa na bei za bidhaa sokoni,
Kushindwa kuongeza mishahara ya watumishi wa umma kwa miaka minne mfululizo ni dalili ya kuonyesha uchumi wetu haukuwi (economic stagnation) au uwekezaji unaofanyika haufanyiki kwa kuangalia umuhimu wa rasilimali watu katika uendeshaji wa uchumi, jambo ambalo linaufanya uwekezaji huo kutokuwa na maana kwa jamii ya watanzania. Tukumbushane moja ya Kauli ya Mwalimu Nyerere kuwa dhana ya maendeleo ya nchi ni lazima ionekane kwa watu na sio kwa vitu.
Maboresho ya maslahi ya watumishi wa umma yameendelea kutegemea Utashi binafsi wa viongozi wa nchi. Hakuna mfumo madhubuti wa kusimamia na kutekeleza mipango inayolinda maslahi ya watumishi ya umma. Kauli za viongozi ni mwiba kwa watumishi wa umma nchini, tukumbuke kwamba kuna chombo cha Serikali ambacho kazi yake ni kujadiliana na vyama vya wafanyakazi kuhusiana na ongezeko la mishahara kwa watumishi, lakini kutokana na udhaifu wa miundo na mifumo ya Serikali taasisi hiyo imekuwa dhaifu kuweza kukutana na kutimiza majukumu yake.
Kwa kurejea kauli ya Rais Mstaafu wa Marekani Baraka Obama kwamba “Africa does not need a strong leaders rather needs strong institutions”. Kauli hiyo inaakisi mazingira ya taasisi zetu moja kwa moja, na kwa muktadha huu ni vyama vya wafanyakazi kuwa dhahifu na hivyo kushindwa kufanya majadiliano yenye tija na Serikali kuboresha maisha ya wafanyakazi.
Aidha, tulitarajia vyama vya wafanyakazi kuwa na takwimu sahihi za nini kinapatikana katika ukusanyaji wa mapato na nini kinatakiwa wafanyakazi wapatiwe kama motisha ya kuongeza ari, lakini kwa bahati mbaya watumishi wameshindwa kufahamu ukweli uko wapi.
Pamoja na kwamba Mheshimiwa Rais amesema kuwa Serikali imeshusha mfumuko wa bei “inflation” kutoka asilimia 6.7% hadi 3.6% lakini bidhaa sokoni zimeendelea kupanda bei. Aidha, wakati anaingia madarakani bei ya dolla ya Marekani kwa shilingi ya Kitanzania ilikuwa ni 1: 2,121.29 sasa hivi May 2018 uwiano ni 1: 2,287.9 hapa ni kweli mfumuko umepungua?
Serikali ya awamu ya tano ilipoingia madarakani sukari ilikuwa inauzwa kwa shilingi 1800/- kwa kilo moja lakini imepanda na kufika shilingi 2,400/- na sasa inauzwa kwa shilingi 3500/-. Mchele umepanda kutoka 1,200/- hadi 2,500/- kwa kilo. Mafuta ya petrol yalikuwa ni shilingi 1,300/- kwa lita sasa hivi ni shilingi 2,250/- kwa lita.
Ukiangalia gharama za vifaa vya ujenzi kwa sasa kwa kulinganisha na ilivyokuwa kwa kipindi cha awamu ya nne, ni dhahiri majibu wananchi wanayo wenyewe.
Ni ukweli kuwa mfumuko anao usema kuwa ameudhibiti ni mfumuko wa bei za vyakula ambao umedhibitiwa kwa kutumia vyombo vya dola lakini si kwa maunufaa ya wakulima. Bei za vyakula zinatakiwa zirekebishwe na mahitaji ya soko. Hapa nchini mazao yamezuiwa kutoka nje ya nchi wakati huo huo ndani ya nchi mzunguko wa fedha hakuna (uwezo wa watu kununua umepungua sana kwa sababu ambazo zinajulikana na wote)
Serikali inasema makusanyo yameongezeka kutoka bilioni 805.6 hadi shilingi trilioni 1.3 kwa mwezi. Ni wajibu wa Serikali kuongeza mishahara ya watumishi wa umma ili waweze kukidhi mahitaji yao.
Watumishi wa umma ndiyo ingini ya Maendeleo na ndio wanaoendesha Serikali, tukumbuke kwamba wafanyakazi (watumishi wa umma) kupitia kodi ya lipa unachopata (PAYE) kwani takribani 75% ya kodi ya mapato hutokana na PAYE na kuwafanya kuwa ndio walipaji wakuu wa kodi kwa Serikali kuliko sekta yoyote ya uchumi na mbali na kodi hiyo kuna makato mengine ya lazima kama vile kodi za mikopo ya chuo, kodi ya veta(SDL), mifuko ya hifadhi n.k. Hivyo basi Serikali kuendelea kuwabana wafanyakazi kwa kutowapandishia mshahara, ina maana kwamba gharama za maisha haziendani na mapato ya watumishi na kodi ni nyingi.
Ugumu wa maisha unaosababishwa na mishahara isiyokidhi mahitaji muhimu “Living wage” una athari zifuatazo;
1. Watumishi kukosa ari na motisha ya kufanya kazi kwa kujituma na kupunguza tija
2. Kuua ubunifu wa watumishi wa umma
3. Kuongezeka kwa maradhi ya sonona (depression) na blood pressure (Bp)
4. Kuacha kazi (mara nyingi wanaondoka ni wafanyakazi mahiri na wabunifu-brain drain) na hivyo kupunguza nguvu kazi
5. Kuanzisha miradi na biashara ndogo ndogo ambazo zitapunguza muda wa kutekeleza majukumu yao kazini.
Kwa hitimisho, kauli hiyo ya Mhe Rais inaonesha jinsi ambavyo awamu hii ya tano haijali watumishi wa umma ambao ndio wanaoendesha Serikali.
Kambi Rasmi ya Upinzani inashauri Serikali kujenga utumishi wenye kujituma, wenye ari ya kufanya kazi na wenye afya ya akili, utumie makusanyo ambayo ni kodi ya watumishi hawa waongezewe mishahara ili kukidhi mahitaji muhimu ili nayo Serikali iweze kufikia malengo iliyojiwekea.
ASANTENI