aliisaac1000
JF-Expert Member
- Jul 11, 2015
- 407
- 272
Naunga mkono kauli ya Mh. Magufuli wakati akimwapisha kamanda sirro ya kuwa afanye 'total overhaul' ya jeshi la polisi. Kwa kusema hivyo naamini pia alikuwa anamaanisha jeshi lifanye kazi kwa mbinu za kisasa na weledi mkubwa pamoja na kutumia busara kuliko ilivyo sasa, kama sikosei 'overhaul' ni pamoja na kubadilika katika utendaji wa majukumu ya jeshi la Polisi ikiwemo;
kuitikia wito pindi wanapohitajika kwenye matukio tofauti na ilivyo sasa wakiitwa wanakuomba ulete gari uje kuwachukua, wa tumie utaalam kwenye upelelezi wa matukio ambao hauta vunja haki za binaadamu kwa kuwaweka watu ndani kwa muda mrefu bila ya ushahidi wa kutosha, kuacha matumizi mabaya ya silaha hususan pale wanapokabiliana na raia ambae dhahiri shahiri hana silaha, mfano ni ya Nape Mnauye n.k, waachane na tabia inayolalamikiwa ya kubambikia watu kesi, waacha pia kukamata watu hovyo hovyo na kujenga chuki kwa kukamata bidhaa zao hovyo hovyo - matakeo ndio hayo ya kibiti kama ni kweli inavyosemekana kuwa moja ya kero.
Pia kikosi cha Traffic police nacho vilevile kifumuliwe ili kiachane na stili ya sasa ya kuwa'TRAFFIC POLICE STATE' ambapo sasa barabarani huwezi kufanya safari ya kikazi kwa ufanisi kwa sababu huwezi kwenda kilometa mbili bila kupigwa mkono, sera ya usalama barabarani kwa sasa ni faini tuu! elimu imepewa kisogo., hii inaongeza chuki ya watu kwa serikali yao. Vipato vya wananchi ni vidogo sana hivyo kumchukulia mtu elfu thelathini sio suala dogo, serikali ielewe kuwa waendesha magari wote sio matajiri, ni mazingira yaliyoko ndio yanatufanya tutumie magari. Tamko la Amiri jeshi mkuu kufanya mabadilo ya jeshi la polisi na amini si kwa maana nyingine yoyote bali kwa maana hiyo niliyoainisha hapo juu.