Kauli ya Mkulo kuhusu EPA: Kikwete vunja ukimya

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,790
288,109
Date::6/29/2008
Kauli ya Mkulo kuhusu EPA: Kikwete vunja ukimya
Na Theodatus Muchunguzi
Mwananchi

WAZIRI wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkulo ametoa kauli ambayo imebadili upepo wa kisiasa nchini. Mkulo anasema kuwa Sh 133 bilioni zilizokwapuliwa na kampuni 22 za kitapeli kutoka Akaunti ya Malipo ya Madeni ya Nje (EPA) katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT) siyo za umma, bali ni za wafanyabiashara.

Mkulo alitoa kauli hiyo wakati akifunga mjadala wa Bejeti ya Serikali ya mwaka 08/09 bungeni mjini Dodoma wiki iliyopita.

Na kilichomsukuma Mkulo kutoa kauli hiyo, inaonyesha ni kutaka kuzima hoja za baadhi ya wabunge walioibana serikali ihakikishe fedha hizo zinarejeshwa pamoja na kuwataja kwa majina watu wote waliohusika na wizi huo.

Baadhi ya wabunge walionyesha msimamo mkali kuhusiana na suala hilo , kiasi cha baadhi ya wabunge, ambao inadaiwa wanatumiwa na watuhumiwa hao kusimama kuwapinga wenzao wanaofuatilia matumizi mabaya ya fedha za serikali.

Wabunge kama Anne Kilango Malecela, ambaye alijifananisha na mmoja wa wanafalsafa wa Ugiriki ya kale ambaye alikuwa bingwa wa mijadala, Socrates na Fred Mpendazoe walitoa hoja nzito za kuibana serikali ichukue hatua zinazostahili katika kuhakikisha fedha hizo za umma zinarejeshwa na watuhumiwa wanatajwa kwa majina.

Kilichowashangaza wengi ni kuona baadhi ya wabunge, mmoja wao Anna Abdallah wakisimama kumshambulia Kilango kuachana na hoja yake na baadaye Mkulo kutoa kauli hiyo, ambayo ni dhahiri imeigawa serikali ya Rais Jakaya Kikwete na pia kuonyesha mashaka kuhusiana na serikali ya Awamu ya Nne inavyoendesha mambo yake.

Tafsiri ya kauli ya Mkulo inamaanisha kuwa serikali ya sasa inaendeshwa bila mfumo, kwa maneno mengine kila aliyeko serikalini anafanya mambo ama anavyoona au anavyotaka. Uendeshaji wa serikali wa aina hii haufai na unaweza kusababisha serikali ya aina hiyo kusambaratika.

Matamshi hayo Mkulo alipaswa kuyatamka baada ya kupata baraka za Baraza la Mawaziri na siyo yeye kama Mkulo kama dhana ya uwajibikaji wa pamoja serikalini inavyotaka. Swali linalobaki katika vichwa vya wengi ni je, Mkulo alitoa kauli hiyo yeye binafsi au alitumwa na serikali?

Mashaka kuhusiana na matamshi yake yanatokana na kuzungumzia jambo hilo tofauti na lilivyozungumziwa kwa umma na Rais Kikwete mapema Januari, mwaka huu. Rais Kikwete baada ya kampuni ya Ukaguzi wa Mahesabu ya Ernest & Young kubainisha wizi wa fedha hizo, alitangaza kumtimua aliyekuwa Gavana wa BoT, marehemu Daudi Ballali na pia kutangaza kuunda Kamati Maalum ya uchunguzi ikiwajumuisha Mkuu wa Jeshi la Polisi, Inspekta Jenerali Said Mwema, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Johnson Mwanyika na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kupambana na Kuondoa Rushwa, (Takukuru), Dk Edward Hosea.

Sababu iliyomlazimisha Rais Kikwete kuunda kamati hiyo ni wizi wa kiasi kikubwa cha fedha za umma ili iwachunguze walioiba fedha hizo kisha kuwakamata na kuwafikisha mbele ya mkono wa sheria. Hicho ndicho alichokisema Kikwete kupitia kwa Katibu Mkuu Kiongozi, Philemon Luhanjo, alipozungumza na waandishi wa habari.

Watanzania walimpongeza Rais Kikwete kutokana na hatua alizozichukua baada ya tukio hilo na walijenga imani naye kuwa ahadi za kuwashughulikia mafisadi hao zitatekelezwa na hivyo wakabaki wakisubiri muda wa miezi sita, ambao Rais Kikwete aliipa kamati hiyo utumie ili mchakato wa hatua hizo uanze.

Lakini kadri ya siku zilivyokuwa zinaenda, mambo kadhaa yamekuwa yakijitokeza. Moja ya mambo hayo ni serikali kuutangazia umma kuwa baadhi ya kampuni hizo za kitapeli zimeanza kurejesha fedha hizo lakini bila kueleza waliozirejesha ni kina nani.

Mkulo mwenyewe ndiye alikuwa mstari wa mbele kutangaza kuwa zaidi ya Sh 50 bilioni zimesharejeshwa na kampuni hizo za kitapeli na kudokeza kuwa serikali ina imani kuwa zaidi ya asilimia 70 zitarejeshwa lakini pia bila kueleza kama fedha hizo zinarejeshwa na riba.

Kisingizio alichokitoa kuhusu watu hao kutotajwa majina ni kuwa fedha hizo zilichukuliwa na kampuni na si watu binafsi. Alikwepa kueleza ni kina nani waliosaini hundi za kuchukua fedha hizo au waliokwenda BoT kuzichukua.

Baada ya Mkulo kusema hayo, alifuatia Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, aliyesema kuwa kuwakamata watuhumiwa wa ufisadi wa EPA ni vigumu kwa sababu ni watu wenye fedha nyingi. Pinda naye alionyesha udhaifu kwa kusahabu kuwa haiwezekani dola ikawatamkia raia kuwa kuna mtu au kikundi cha watu chenye nguvu zaidi yake.

Kilichofuatia wiki iliyopita ni matamshi tata ya Mkulo kuwa fedha hizo hazikuwa mali ya umma bali wafanyabiashara. Kama hazikuwa fedha za umma, kwa nini Rais Kikwete aliunda kamati ya uchunguzi? Ninachofahamu ni kuwa waliokuwa wanaidai serikali ni wafanyabiashara walioagiza bidhaa miaka iliyopita wakati wa matatizo ya uchumi kwa niaba ya serikali na baadaye serikali kuwalipa gharama zao pamoja na motisha.

Kwa maana hiyo hakuna mantiki yoyote ya kusema fedha hizo zilikuwa mali ya wafanyabiashara kwa kuwa fedha hizo zilikuwa mali ya umma na zilipaswa kulipwa kwa wafanyabiashara halali, ambao ni kweli waliagiza bidhaa hizo. Mkulo anashangaza kwa sababu kwa makusudi ama kutojua anawatetea wafanyabiashara ambao ni haramu kwa kuwa hawa hawakuagiza na kuingiza bidhaa, bali watu hao waliibuka na kampuni zao za kitapeli na kukwapua fedha hizo.

Suala hili linaonekana kuwa na ugumu kutokana na mamlaka za juu za serikali kutofautiana. Nasema hivyo nikimaanisha kuwa anachokisema Mkulo kinapingana na wakubwa wake Rais Jakaya Kikwete na Luhanjo. Wananchi wanabaki wakijiuliza nani anasema ukweli na nani ni mwongo na kwa sababu zipi?

Lakini kwa Watanzania wengi wanaofuatilia mwenendo wa siasa nchini watakubaliana nami kuwa suala hili linashughulikiwa kwa maslahi binafsi badala ya maslahi ya umma. Tunasikia kuwa watuhumiwa wa ufisadi huo ni wafanyabiashara na wanasiasa na kwamba wamekuwa wanafanya vikao mbalimbali vya kuweka mikakati ya kulizima suala hilo.

Inawezekana ndiyo sababu tunasikia watuhumiwa wa kashfa mbalimbali wanaanza kusafishwa na wabunge vibaraka. Kama wanasafishwa bungeni bila shaka na mamlaka nyingine zina mipango ya kuwasafisha.

Matokeo ya mwenendo huo mwishowe yanaweza kuathiri matokeo ya kamati ya Rais Kikwete kuhusu wizi wa mabilioni ya EPA, ambapo taarifa ya uchunguzi huo tunaitarajia itakamilika mwezi huu.

Kama serikali inaanza kutoa kauli za kuwasafisha mafisadi wa EPA kama ya Mkulo kabla ya akina Mwayika, Mwema na Hosea kuwasilisha matokeo ya uchunguzi, maana yake ni kuwa itatoa ushawishi kwa kamati hiyo kuwasilisha kile ambacho serikali inataka wananchi wakiamini.

Siyo siri kwamba hivi sasa yanasemwa mambo mengi mitaani kuhusiana na wizi wa mabilioni ya EPA. Wapo wanaodai kuwa Mkulo anazungumza kwa kujiamini kwa kuwa ametumwa na baadhi ya wakubwa wake kuweka msimamo huo kabla matokeo ya uchunguzi kutangazwa.

Ili kuwarejeshea wananchi imani kwa Rais Kikwete na kuondoa taarifa za uvumi, itakuwa vizuri na busara kwa Rais kutoa ufafanuzi kama fedha zilizokwapuliwa BoT ni za umma au za wafanyabiashara. Kulizungumzia mwenyewe bila kuwatumia wasaidizi wake kutaondoa utata uliopo.

Baruapepe: theodatusm@yahoo.com

Simu: 0737038475
 
Jamani kuna watu walishasema hapa jamvinikwamba baada ya kufa Balali, sasa kauli za serikali lazima zitaanza kutoka na tena controversial stories.
Haya ndiyo tunaanza kusikia na kwa kweli watasema mengi hata watasahau waliyosema mwanzoni.
Si unakumbuka hata Meghji alijichaganya hivyo hivyo? yeye alisema zilitumika kwa usalama wa taifa. Hii ni aibu tupu kwa uongozi wa nchi hii.
 
Jamani kuna watu walishasema hapa jamvinikwamba baada ya kufa Balali, sasa kauli za serikali lazima zitaanza kutoka na tena controversial stories.
Haya ndiyo tunaanza kusikia na kwa kweli watasema mengi hata watasahau waliyosema mwanzoni.
Si unakumbuka hata Meghji alijichaganya hivyo hivyo? yeye alisema zilitumika kwa usalama wa taifa. Hii ni aibu tupu kwa uongozi wa nchi hii.

JK naye kawa BUBU, hajui aegemee upande gani katika vita kali inayoendelea ndani ya bunge kati ya watetezi wa maslahi ya Watanzania na watetezi wa mafisadi maana watakaoshinda katika vita hiyo ndiyo watakaoshika 'utamu' ndani ya CCM sasa jamaa anasubiri aone upepo utaelekea wapi ili naye aunge behewa lake. Kiongozi asiye na msimamo kama JK hafai kabisa, maana yeye kama kiongozi wa chama ndiye aliyetakiwa atoe muongozo ndani ya chama chake lakini amekaa pembeni kabisa kama hayamuhusu!!!!
 
Hata kama ni za wafanya biashara ,kinachojulikana kuwa zilikuwa ndani ya udhibiti wa Serikali ,na ijukane wazi kuwa tatizo sio kuchukuliwa fedha hizo ,kwani utaratibu wa kuchukuwa fedha upo duniani kote na watu wanachukua zaidi ya hicho kilichochotwa hapa Tz ,ifahamike kuwa njia na utaratibu wa kuchukua fedha hizo haukufuatwa vilivyo,mikataba ya uchukuaji na urudishaji wa fedha hizo haujulikani na zaidi makampuni yaliopewa fedha hizo mengine hayapo.
Je hawa mliokuwa mkiwasema wameanza kurudisha fedha hizo kama mnadai ni fedha za wafanya biashara ilikuwaje wakaanza kuzirudisha na kila siku mnasema zimeanzwa kurudishwa ,Je kauli zile zilikuwa ni gelesha tu ?Ludisheni feza yetu msilete ngebe au na wewe unaetetea utakuwemo au umeshaahidiwa vijisenti ikiwa utafanikiwa kuzima .
 
Somebody has to take one 4 the team... JK should be be the one to bring all to justice who are guilty of UFISADI and we will forever remember him for his courage if he does and we shall forever condem him 4 his cowardice if he does not.
 
kwani Kitu Gani Msichoelewa Wajameni???? Fedha Za Epa Zilitumika Kumweka Madarakani Jk Pamoja Na Team Yake....na Hao Wapambe Wake Wamefaidika Nazo Sana Na Wanaendelea Kufaidika Nazo...wengine Wapo Madarakani, Wengine Wanakula Raha Zao Kivingine....sasa Mnataka Yeye Afanye Kitu Gani Hapo???mnafikiri Ataweza Kuwafanya Lolote Wenzie? Aaagh! Thubutu!! Kwa Hili Na Mengineyo Ya Dizaini Hii Tukubali Maumivu!!!...nawashangaa Mnaotegemea Jk Afanye Kitu Chochote Cha Maana..mnapoteza Muda Na Nguvu Zenu Bure!!!
 
Back
Top Bottom