Kauli ya Membe imenishangaza

Kauli ya Membe imenishangaza

katika mkutano wake wa kutangaza nia huko lindi membe alitoa kauli ambayo imenishangaza pale aliposema "enzi za mwalim ilikua mtoa rushwa na mpokea rushwa wote wanawajibishwa nitakapo kua raisi itakua kinyume mimi nitamwajibisha mpokea rushwa na mtoa rushwa ni tamwachia" kiukweli hasa hapo pa kumwachia mtoa rushwa ndipo pameniacha mdomo wazi.
kwasababu hata hawa wanasiasa wanao toa rushwa za chumvi na sukari kwenye uchaguzi inamaana membe ata waacha na kwenda kushika raia ambao wamepokea vitu hivyo?
ina maana watu kama Ruge malira wanao honga vigogo wataachiwa? Wadau hii kauli ina faa kumpa membe urais?

Hela za gadaf akirudisha tutampa bigup vinginevyo ngonjera zake hazina mapokeo
 
Hizo ni fikra za kitoto sana tena za std 7 kama sijakosea yaani unafikiria tu kichwani na kuhisi ndio njia sahihi kumbe kiuharisia ni ngumu na ni kitu si cha afya kiutendaji hasa ktk hali ya kushughurikia usawa baina ya watu wazito na wepesi
 
hata mimi kwa muda mrefu nilikuwa naishangaa hii sheria. Mtoa rushwa anashurutishwa kwanini yeye asiwe shahidi
 
Hivi Membe anaelewa kwamba rais hatungi sheria?
 
Mkuu raisi hana uwezo wa kubadili katiba. Akishaapa kuilinda anailinda hana mamlaka ya kuibadili,ni bunge peke yake ndio lenye uwezo huo kisheria.
Ok. Uko sahihi. Nilikuwa na maana kuwa Rais aliye madarakani anaweza kuanzisha mchakato wa kuibadili kama ilivyotokea hapa kwetu. Bila Kikwete kutangaza kuanzisha mchakato huo kusingekuwa na uandikaji wa katiba mpya.
 
Membe pia aliniacha hoi aliposema ndani ya miaka kumi ya uongozi wake, wapinzani ataumaliza upinzani moja kwa moja!

Hii maana yake ni kwamba hataki ushindani wa kisiasa. Na hata wapinzani ndani ya Chama chake wenye mawazo tofauti na yake watashughulikiwa. Kauli hii ina maana kuwa akitawala ndiyo mwanzo wa kifo cha democrasia Tanzania.
 
ccm delite MEMBE delite LOWASA,kwa mustakari wa taifa letu,na mkiwapitisha hawa zambi hii ccm lazima ife.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom