Kauli ya Membe imenishangaza

Kauli ya Membe imenishangaza

Jaji matundu

JF-Expert Member
Joined
Mar 6, 2014
Posts
251
Reaction score
92
katika mkutano wake wa kutangaza nia huko lindi membe alitoa kauli ambayo imenishangaza pale aliposema "enzi za mwalim ilikua mtoa rushwa na mpokea rushwa wote wanawajibishwa nitakapo kua raisi itakua kinyume mimi nitamwajibisha mpokea rushwa na mtoa rushwa ni tamwachia" kiukweli hasa hapo pa kumwachia mtoa rushwa ndipo pameniacha mdomo wazi.
kwasababu hata hawa wanasiasa wanao toa rushwa za chumvi na sukari kwenye uchaguzi inamaana membe ata waacha na kwenda kushika raia ambao wamepokea vitu hivyo?
ina maana watu kama Ruge malira wanao honga vigogo wataachiwa? Wadau hii kauli ina faa kumpa membe urais?
 
Kwani sheria ya sasa kikatiba inasemaje au yeye atabadili hicho kipengele cha sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa, but nahisi yupo kwenye namna nyingine ya mwendelezo wa siasa....
 
Huku mwelewa MH. Membe.Hoja ni kwamba unapowaweka wote wanahatia inakuwa ni vigumu kuchunguza kesi kwani wote wawili wataficha ili ukweli usijulikane.

Lakini uki mvictimize mpokea rushwa then mtoa rusha atakuwa tayari ku cooperate na vyombo husika ili kumtia hatiani aliyepokea rushwa.

Hii ni kwa sababu kwa rushwa zilizo nyingi mpokea rushwa ndo chanzo. Mtoa rushwa anakuwa hana namna. Analazimika kutoa ili mambo yake yaende huku akiumia moyoni. Sasa kwa sheria ya rushwa ya sasa mtoa rushwa akienda kutoa taarifa na yeye anaingia matatani ndo maana vitendo vingi vya rushwa haviwi reported.
 
katika mkutano wake wa kutangaza nia huko lindi membe alitoa kauli ambayo imenishangaza pale aliposema "enzi za mwalim ilikua mtoa rushwa na mpokea rushwa wote wanawajibishwa nitakapo kua raisi itakua kinyume mimi nitamwajibisha mpokea rushwa na mtoa rushwa ni tamwachia" kiukweli hasa hapo pa kumwachia mtoa rushwa ndipo pameniacha mdomo wazi.
kwasababu hata hawa wanasiasa wanao toa rushwa za chumvi na sukari kwenye uchaguzi inamaana membe ata waacha na kwenda kushika raia ambao wamepokea vitu hivyo?
ina maana watu kama Ruge malira wanao honga vigogo wataachiwa? Wadau hii kauli ina faa kumpa membe urais?

Sababu kubwa ya MEMBE kufanya hivyo ni kwasababu ya Mabadiliko ya SHERIA ZINAZOIONGOZA NCHI HII TOKA UHURU... Kwa Sasa hivi tangu nchi ikumbatie WawekezaJI wa GAS and OIL Siasa za Serikali ya CCM zimekuwa za KIBEPARI...

Hence, Mara nyingi Capitalist Nation haimshitaki Capitalist Mwenzake isipokuwa wale Uchwara Money Mongers; Greedy etc
 
katika mkutano wake wa kutangaza nia huko lindi membe alitoa kauli ambayo imenishangaza pale aliposema "enzi za mwalim ilikua mtoa rushwa na mpokea rushwa wote wanawajibishwa nitakapo kua raisi itakua kinyume mimi nitamwajibisha mpokea rushwa na mtoa rushwa ni tamwachia" kiukweli hasa hapo pa kumwachia mtoa rushwa ndipo pameniacha mdomo wazi.
kwasababu hata hawa wanasiasa wanao toa rushwa za chumvi na sukari kwenye uchaguzi inamaana membe ata waacha na kwenda kushika raia ambao wamepokea vitu hivyo?
ina maana watu kama Ruge malira wanao honga vigogo wataachiwa? Wadau hii kauli ina faa kumpa membe urais?

Huyu Membe alishajitoa kwenye kampeni aliposema atampigia debe Mwandosya, sasa kwa ninibwatu wanaendelea kumsikikiza kama mgombea urais wakati yeye mwenyewe ana mtu wake anayetaka awe rais?

Mtu haekewi hata maneno gani yanatakiwa kusemwa na maneno gani hata kama unayafikiri hutakiwi kusema anawezaje kuwa rais?
 
hilo ndo tatizo la kutumwa na kundi fulan kugombea nafas kubwa kama urais kisa kumpunguza nguvu lowassa...aaaaaaaa tanzania bhana dats why outsiders are laughing at us!
 
Membe pia aliniacha hoi aliposema ndani ya miaka kumi ya uongozi wake, wapinzani ataumaliza upinzani moja kwa moja!

Hii maana yake ni kwamba hataki ushindani wa kisiasa. Na hata wapinzani ndani ya Chama chake wenye mawazo tofauti na yake watashughulikiwa. Kauli hii ina maana kuwa akitawala ndiyo mwanzo wa kifo cha democrasia Tanzania.
 
Huku mwelewa MH. Membe.Hoja ni kwamba unapowaweka wote wanahatia inakuwa ni vigumu kuchunguza kesi kwani wote wawili wataficha ili ukweli usijulikane.

Lakini uki mvictimize mpokea rushwa then mtoa rusha atakuwa tayari ku cooperate na vyombo husika ili kumtia hatiani aliyepokea rushwa.

Hii ni kwa sababu kwa rushwa zilizo nyingi mpokea rushwa ndo chanzo. Mtoa rushwa anakuwa hana namna. Analazimika kutoa ili mambo yake yaende huku akiumia moyoni. Sasa kwa sheria ya rushwa ya sasa mtoa rushwa akienda kutoa taarifa na yeye anaingia matatani ndo maana vitendo vingi vya rushwa haviwi reported.
si kweli mtoa rushwa ukitoa taarifa unatiwa matatani.ukitoa taarifa za kuombwa rushwa unapewa hela zao ili wamkamate mpokeaji.tatizo pccb ukiwapa taarifa kama wanamjua wanamtonya muhusika unabaki unaumbuka.
 
Mie nitasimamia mantiki ya kauli hiyo bila kujali aliyeimtoa. Hebu fikiria, mkeo mjamzito, unapofika hospitali unazinguliwa, unaombwa hela ili fanyiwe upasuaji. Unaonaona sio haki, unatoka hospitali unaenda pccb unaripoti, wanakuja wanaweka mtego, unatoa hela dakatari aliyetakiwa kumfanyia mkeo upasuaji anakamatwa. Mkeo anafariki wakati wewe ukitekeleza sheria ya nchi. Sawa hiyo? Ilitakiwa utoe hiyo rushwa kwanza, upasuaji ufanyike halafu uripoti ili daktari ashughulikiwe, wewe ukiwa shahidi kuwa kutoa ile rushwa. Hiyo ndio mantiki. Kubadili sheria sio dhambi. Rais anapoapa anaapa kulinda katiba iliyopo kwa wakati huo anapoapa. Akishaapa hata hiyovkatiba anaweza kuibadili.
 
Well said!
 
Mkuu raisi hana uwezo wa kubadili katiba. Akishaapa kuilinda anailinda hana mamlaka ya kuibadili,ni bunge peke yake ndio lenye uwezo huo kisheria.
 
watu wa Arusha walishakosa imani na Membe pale alipowadanganya wakaaji wa nyumba za Soweto matokeo yake nyumba hizo zimevunjwa miaka mitano imepita hapajafanyiwa kitu yoyote
 
Huyu Membe alishajitoa kwenye kampeni aliposema atampigia debe Mwandosya, sasa kwa ninibwatu wanaendelea kumsikikiza kama mgombea urais wakati yeye mwenyewe ana mtu wake anayetaka awe rais?

Mtu haekewi hata maneno gani yanatakiwa kusemwa na maneno gani hata kama unayafikiri hutakiwi kusema anawezaje kuwa rais?

Tusisikilize maneno kijuujuu tu bali tunatakiwa tusome between the lines. Hiyo kauli yake kumuunga mkono pro mwandosya mi naona ni sahihi kwa sababu kubwa mbili.
Ya kwanza ni katika mbio zozote lazma kutakuwa na mshindi na wale ambao watapoteza, sasa kama wewe ni mshindani basi lazma ukubali kwamba kuna kushindwa pia. Kauli hiyo kwangu namuona kama ni kiongozi asiye na uchu wa madaraka na mtu. Kuna mtangaza nia mwengine alisema kwamba yeye hana mpango wa kupoteza je akipoteza atafanya nini, kauli kama hizi ni hatari kwa amani yetu.
Point ya pili ni kwamba jamaa hafuati mkumbo kussupport mwana saisa yoyote ilimradi amamsupport mtu au kuangalia uhakika wa kushinda ili awe kwenye position nzuri. Mi naona ana misingi yake ya kumchagua mwandosya. Kwanza mwandosya ni mtu safi muadilifu na ndiyo aina ya kiongozi ambaye anatakikana. Hiyo inamaanisha membe hawezi kuungana na mafisadi.
 
Yaan jamaa kwa kauli hiyo anaonekana amechanganyikiwa! Yaan siku ile aliongea kama mganga wa kienyeji!
 
...atakuwa rais wa umoja wa kufa na kuzikana bhaaas, nchi asahauu kuanzia Leo.....
 
Huku mwelewa MH. Membe.Hoja ni kwamba unapowaweka wote wanahatia inakuwa ni vigumu kuchunguza kesi kwani wote wawili wataficha ili ukweli usijulikane.

Lakini uki mvictimize mpokea rushwa then mtoa rusha atakuwa tayari ku cooperate na vyombo husika ili kumtia hatiani aliyepokea rushwa.

Hii ni kwa sababu kwa rushwa zilizo nyingi mpokea rushwa ndo chanzo. Mtoa rushwa anakuwa hana namna. Analazimika kutoa ili mambo yake yaende huku akiumia moyoni. Sasa kwa sheria ya rushwa ya sasa mtoa rushwa akienda kutoa taarifa na yeye anaingia matatani ndo maana vitendo vingi vya rushwa haviwi reported.

kwani sasa hivi ukiombwa rushwa na ukienda takukuru kutoa taarifa je????Inakuaje
Membe kajichanganya tu
 
katika mkutano wake wa kutangaza nia huko lindi membe alitoa kauli ambayo imenishangaza pale aliposema "enzi za mwalim ilikua mtoa rushwa na mpokea rushwa wote wanawajibishwa nitakapo kua raisi itakua kinyume mimi nitamwajibisha mpokea rushwa na mtoa rushwa ni tamwachia" kiukweli hasa hapo pa kumwachia mtoa rushwa ndipo pameniacha mdomo wazi.
kwasababu hata hawa wanasiasa wanao toa rushwa za chumvi na sukari kwenye uchaguzi inamaana membe ata waacha na kwenda kushika raia ambao wamepokea vitu hivyo?
ina maana watu kama Ruge malira wanao honga vigogo wataachiwa? Wadau hii kauli ina faa kumpa membe urais?
Ulisikiliza nusu wewe, alisema kama mtoa rushwa atatoa taarifa ya kuombwa rushwa ataachwa na kuwajibishwa aliyeiomba
 
Mpokea rushwa siku zote ndiyo mwisho wa siku anafanya maamuzi ambayo yana athari mbaya kwa taifa au wananchi wake. Hao walopokea rushwa kutoka kwa ruge wengi wako serikalini ambapo wana ethics zinazowaendesha kwa maana kwamba wasipo fuatisha zile ethics tayari taifa linahujumika na athari zake zinaaffect hadi mtu wa chini. So ni sawa kabisa kuwabana wapokea rushwa zaidi.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom