Kwanza kwa Lema, ulipotaka kutoa ushahidi kuwa Pinda kadanganya bungeni spika akakataa usilonge mjengoni bali mkaonane 'faragha' na huko umpe mambo yako. Na Lissu pia majuzi nimekuona umeng'aka na Ngeleja kudanganya na wewe pia umealikwa 'faraghani' ukampe spika mambo yako; sasa swali - huko faraghani mlifanya nini na matokeo yake ni yapi? Maana huu utakuwa uhuni sasa, waziri anadanganya na nyinyi mambo mnamalizia faraghani.Naombeni jibu hapa jukwaani. Mbona Zitto aliposhambulia uongo wa Karamagi alipigwa chini vikao kibao na hakuitwa faraghani? au ni kwa sababu enzi zile spika hakuwa mwanamama?