Kauli ya kuhamia benki moja kubwa Tanzania iliyotolewa katika ziara ya kusini ya mkuu

undugukazi

JF-Expert Member
Sep 15, 2011
315
82
Niwatoe hofu wanajamii wote, hakuna sheria wala katiba duniani inayomlazimisha mtu kuhamia benki moja kwenye nchi, katika biashara kila mtu ana test zake, benki aliyoitaja mkuu wapo wanaoipenda na wapo walioichoka, na hii inatokea kila mahali duniani,

Kifupi kama haja zako zitatimizwa kwa kuingia benki hiyo ingia ila usije ingia kwa ushauri wa mtu ukakuta pakavu, binafsi napenda benki zinazochipukia nikiwa na vi m vitano tshs5000000 nakuwa mteja mkubwa kwao na branch manager ananipigia simu kunipa taarifa za akaunti yangu, nikifika sipangi foleni,

kwanza benki zinazochipukia hazinaga foleni kabisa sielewi mtu pesa yako umetoa jasho mwenyewe unaenda itoa kwa foleni sio kwa tela hadi atm kote foleni, ila simaanishai uniigie mimi, mimi sipendi shida ila napenda kuthaminiwa ndio maana naenda vibenki vidogo vinavyokubali hata niweke friji rehani vinipe mkopo na ukiweka kagari ndio kabisa unapa limkopo la maana (uwe na chanzo tu cha maana cha kulipa mkopo).

kwahiyo nimeona niweke hili wazi hakuna benki tanzania inayoweza hudumia nchi nzima lazima tutumie benki nyingi na kila moja ina ubora na udhaifu wake katika kujenga taifa la viwanda kuna haja ya kuthamini mchango wa kila benki,

tanzania ina benki zaidi ya 45 kwa sasa na kila benki inalipa kodi zote zinazoenda kwenye pato la taifa moja kwa moja sasa zikikosa biashara (which is impossible) zikafungwa hizi inamana nchi itakosa pato kubwa sana , kodi ya benki moja kubwa haiwezi kufikia kodi ya benki zote zilizobaki, suala la hisa ni utashi wa mwekezaji hata raia wengi wamewekeza kwenye hizo benki kubwa na tunafurahi zikifanya vyema ili tulipwe gawio lakini haimaanishi niitumie kwenye kila shughuli zangu, pia ajira kwa kila benki ni kubwa wakati huo huo wafanyakazi wanalipa p.a.y.e (si chini ya asilimia 30) ambayo hainaga negotiations ni clean money kwenye pato la serikali, pia wanachangia social funds ( asilimia 20 kwa kila mfanyakazi toka kwenye mshahara wake na nyongeza ya mwajiri) zinazotumika kuwekeza kwenye mapinduzi ya viwanda,

naamini wengi mlio na akaunti kwenye mabenki makubwa na vipesa vyenu vidogo hamjawahi onja hata vimkopo na mmekomaa, kuweni na fikra huru benki ni nyingi na zipo zinazotoa hadi riba nzuri kwenye akaunti za matumizi ya kawaida na zile za kusevu. fanyeni tafiti tu.

na biashara ya benki tanzania ipo salama na huru sana hata kama benki ina tawi moja inakuwa chini ya ulinzi mkali wa sheria mubashara za benki kuu ya tanzania, epuka kufuata mkumbo na usijichoshe kwa kupanga foleni zisizo na lazima, tumia tekinolojia, au jiunge benki zenye foleni chache zinazopatikana kwenye mazingira yako, zote zipo salama.
 
mkuu tumekuelewa sana..

yule jamaa ndo alivyo.kila kitu anakiingelea tena bila hata mawazo ya kisomi..
 
mkuu tumekuelewa sana..

yule jamaa ndo alivyo.kila kitu anakiongelea tena bila hata mawazo ya kisomi..
 
Wazo safi.
Bank chipukizi zina ofa ni hatari
 
Naomba kufahamu benki mojawapo ambayo ni chipukizi na ofa zinazotolewa na benki hiyo, naweza kuvutiwa na mimi
Fanya research bank za 2008 and above...equity. fnb. Uba. Ecobank , benki ya wachina, canara, ubl. Hamna foleni huko na huduma ni zile zile.
 
Back
Top Bottom