Kauli ya awali kuhusu kikao cha leo THBUB

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2015
Posts
14,242
Reaction score
34,917
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kinapenda kutoa taarifa ya awali ili kuweka kumbukumbu sawa kuhusu kikao kilichokuwa kimeitishwa na Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB), kabla ya kuahirishwa hadi hapo kitakapoitishwa tena.

Kama ilivyotaarifiwa siku chache zilizopita kupitia vyombo kadhaa vya habari na njia zingine za upashanaji habari, THBUB iliandika barua kuitisha kikao leo Agosti 10, 2016, katika ofisi za tume hiyo jijini Dar es Salaam.

Wajumbe wa kikao hicho walialikwa kwa majina na nafasi yao na kwa mujibu wa barua ya wito kutoka THBUB, walikuwa ni wafuatao;

1. Mhe. George Masaju (MB)
Mwanasheria Mkuu wa
Serikali

2. Jaji Francis S.K. Mutungi
Msajili wa Vyama

3. Mr. Abdulrahman Kinana
Katibu Mkuu CCM

4. Dr. Vincent Mashinji
Katibu Mkuu CHADEMA

5. Katibu Mkuu
Tanzania Centre for
Democracy

6. Bw. Ernest Jumbe Mangu
(IGP)
Mkuu wa Jeshi la Polisi
Tanzania

Kwa mujibu wa barua ya wito, dhumuni kuu la kikao ilikuwa ni kujadili "MUSTAKABALI WA MIKUTANO NA MAANDAMANO YA VYAMA VYA SIASA". Vile vile THBUB ilipenda kujadili tangazo la CHADEMA kuhusu kile kinachoitwa "Ukuta" na mikutano iliyopangwa kufanyika tarehe 01 Septemba, 2016 nchi nzima.

CHADEMA ilihudhuria kikao hicho mahali na muda kama ilivyoelezwa kupitia barua ya wito, ikiwakilishwa na Katibu Mkuu Dkt. Mashinji aliyeambatana na wasaidizi wawili.

Hadi muda ambao kikao kilipaswa kuanza, ukumbini kulikuwa na wajumbe 3 pekee ambao ni, Mwenyekiti wa THBUB Bahame Nyanduga, Dkt. Mashinji na Jaji Mutungi.

Baada ya mazungumzo kati ya wajumbe hao watatu, ikakubalika kuwa kikao kiahirishwe kwa sababu kisingeweza kufanyika na kufikia makubaliano au maazimio yoyote yale, huku upande wa Serikali (Mwanasheria Mkuu na IGP) ukiwa haupo, pamoja na CCM.

Wajumbe waliokuwepo walikubaliana kuwa aliyeitisha kikao (THBUB) aandae kikao kingine pamoja na utaratibu (modality) wa kuwakutanisha wajumbe hao tena.

Kupitia taarifa hii ya awali, Chama kinapenda kutaarifu umma wa Watanzania ambao wanafuatilia mijadala ya ujenzi wa demokrasia nchini na kupigania haki zao, ikiwemo operesheni ya UKUTA inayoendelea nchi nzima sasa kuelekea siku ya Septemba 1, kuwa; hakukuwa na makubaliano au maazimio juu ya jambo lolote kadri ya madhumuni ya kuitishwa kwake, kwa kuwa kimsingi kikao hakikufanyika hadi hapo (iwapo) kitakapoitishwa tena.

Tumaini Makene

Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano
CHADEMA
 
Nini shida hata hawajajitokeza kwenye hicho kikao
 
Sidhani kama CCM wanahoja za kuweza kuwakirisha kwenye kikao hicho kwa kuwa wao ndio waliosababisha yote hayo,labda watakuja kwa kujizoazoa baada ya kukusanya tuhoja twa hapa na pale.
 
nawapongeza CDM kwa kupenda majadiliano. hongereni sana. tunaomba ccm waliige hili kwa maslahi mapana ya taifa letu....
 
Duuh,yani hata mwanasheria mkuu wa selikali hajatokea?,au alihisi lissu atakuepoo!
 
Eti "anayefanya mikutano ya hadhara anachelewesha maendeleo". Kwani huyu hajawahi kuisoma katiba ya Jamhuri au ndo ameamua kujitoa ufahamu ili kuhalalisha udikteta uchwara? Lissu kimbiza huyu mtu hadi aombe po.
 
Hawa wamekaa kishari tu...hoja watatoa wapi wakati wao ndo wavurugaji wa amani. Amani umekuwa mwanvuri wakujitwalia madaraka kwa nguvu za dola.
 
Sidhani kama CCM wanahoja za kuweza kuwakirisha kwenye kikao hicho kwa kuwa wao ndio waliosababisha yote hayo,labda watakuja kwa kujizoazoa baada ya kukusanya tuhoja twa hapa na pale.

Lazima hawa ccm tuwakunde
 
Eti "anayefanya mikutano ya hadhara anachelewesha maendeleo". Kwani huyu hajawahi kuisoma katiba ya Jamhuri au ndo ameamua kujitoa ufahamu ili kuhalalisha udikteta uchwara? Lissu kimbiza huyu mtu hadi aombe po.

Kuna ka ugonjwa kanamsumbua na tiba yake ni kumshikisha ukuta.
 
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kinapenda kutoa taarifa ya awali ili kuweka kumbukumbu sawa kuhusu kikao kilichokuwa kimeitishwa na Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB), kabla ya kuahirishwa hadi hapo kitakapoitishwa tena.

Kama ilivyotaarifiwa siku chache zilizopita kupitia vyombo kadhaa vya habari na njia zingine za upashanaji habari, THBUB iliandika barua kuitisha kikao leo Agosti 10, 2016, katika ofisi za tume hiyo jijini Dar es Salaam.

Wajumbe wa kikao hicho walialikwa kwa majina na nafasi yao na kwa mujibu wa barua ya wito kutoka THBUB, walikuwa ni wafuatao;

1. Mhe. George Masaju (MB)
Mwanasheria Mkuu wa
Serikali

2. Jaji Francis S.K. Mutungi
Msajili wa Vyama

3. Mr. Abdulrahman Kinana
Katibu Mkuu CCM

4. Dr. Vincent Mashinji
Katibu Mkuu CHADEMA

5. Katibu Mkuu
Tanzania Centre for
Democracy

6. Bw. Ernest Jumbe Mangu
(IGP)
Mkuu wa Jeshi la Polisi
Tanzania

Kwa mujibu wa barua ya wito, dhumuni kuu la kikao ilikuwa ni kujadili "MUSTAKABALI WA MIKUTANO NA MAANDAMANO YA VYAMA VYA SIASA". Vile vile THBUB ilipenda kujadili tangazo la CHADEMA kuhusu kile kinachoitwa "Ukuta" na mikutano iliyopangwa kufanyika tarehe 01 Septemba, 2016 nchi nzima.

CHADEMA ilihudhuria kikao hicho mahali na muda kama ilivyoelezwa kupitia barua ya wito, ikiwakilishwa na Katibu Mkuu Dkt. Mashinji aliyeambatana na wasaidizi wawili.

Hadi muda ambao kikao kilipaswa kuanza, ukumbini kulikuwa na wajumbe 3 pekee ambao ni, Mwenyekiti wa THBUB Bahame Nyanduga, Dkt. Mashinji na Jaji Mutungi.

Baada ya mazungumzo kati ya wajumbe hao watatu, ikakubalika kuwa kikao kiahirishwe kwa sababu kisingeweza kufanyika na kufikia makubaliano au maazimio yoyote yale, huku upande wa Serikali (Mwanasheria Mkuu na IGP) ukiwa haupo, pamoja na CCM.

Wajumbe waliokuwepo walikubaliana kuwa aliyeitisha kikao (THBUB) aandae kikao kingine pamoja na utaratibu (modality) wa kuwakutanisha wajumbe hao tena.

Kupitia taarifa hii ya awali, Chama kinapenda kutaarifu umma wa Watanzania ambao wanafuatilia mijadala ya ujenzi wa demokrasia nchini na kupigania haki zao, ikiwemo operesheni ya UKUTA inayoendelea nchi nzima sasa kuelekea siku ya Septemba 1, kuwa; hakukuwa na makubaliano au maazimio juu ya jambo lolote kadri ya madhumuni ya kuitishwa kwake, kwa kuwa kimsingi kikao hakikufanyika hadi hapo (iwapo) kitakapoitishwa tena.

Tumaini Makene

Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano
CHADEMA
Kifupi maandamano yamepigwa marufuku na kama nyie ni wamba jaribuni kuandamana.
 
Mbona kuna TETESI kuwa wajeda wale wanaovaa nguo za mabakamabaka ambao nao ni wananchi wa nchi hii pia wanaunga mkono maandamano hayo? Jee wakishiriki nao hao vijana wa Ernest wataweza kweli kuleta fyoko? Maana tumekuwa tukiona hao vijana wa Ernest wakizabwa makofi barabarani na hawana la kufanya?
Hii itakuwa kama ile style ya kule kwa Farao wajeda walikuwa barabarani kuwa linda ndugu zao raia wasiguswe mpaka Hosein akaondoka na anaishi kwenye cage sasa hivi kama ngegere wa kufugwa. Uncle Davis anawaangalia tuu
 
We MUNGU mwingi wa Rehema na UPENDO nakuomba utuepushe na kikombe hiki ikiwezekana, naomba umtie macho ya rohoni RAISI WETU MPENDWA JOHN POMBE MAGUFULI aone huruma, huku tunakoelekea kivuli cha Giza kinatunyemelea yeye ndie taa ya kuliongoza taifa hili, turudi na kusimamia KATIBA yetu tukufu na SHERIA ZETU NZURI ZIHESHIMIWE. Naamini hakuna linaloshindikana chini ya jua, KIONGOZI AKIANGUKA WOTE WAMFUATAO WATAANGUKA ANGUKO KUU, NAAMINI WOTE KWA NAFASI ZETU TUNA NAFASI ZA KUTUFANYA TUSIMAME PAMOJA KAMA TAIFA NA MUNGU ATATUSIMAMISHA. MH JPM TUNAKUTEGEA ULISEMA HUTATUANGUSHA, USITUANGUSHE KWA HILI. MUNGU AKUBARIKI.
 
Asante, ili maombi yako yapokelewe ombea na Chadema pia waache chokochoko.
 
Back
Top Bottom