Muke Ya Muzungu
JF-Expert Member
- Jun 17, 2009
- 3,444
- 265
Serikali yetu sikivu ya CCM imekataa kutusikiliza kwa kumwajibisha waziri kama Muhongo kutokana na kauli zake chafu na zenye utata. Muhongo ni janga. Hawa ni baadhi ya mawaziri ambao inabidi watoswe ili kukinusuru CCM kushinda 2015.................Hizi ni baadhi ya kauli hatari sawa na za Mwigulu
"Mimi Sikuomba uwaziri, nilibembelezwa kuwa waziri. Bw. Mimi nina kazi yangu inayotambulika kimataifa kule Pretoria. Nikitoka hapa leo narudi kwenye kazi yangu"
Kuna watu watu wanazunguka nchini wakisema kwamba bomu la ajira kwa vijana linakuja kulipuka. Hilo bomu litalipukia kwenye majumba yao na wake zao.....Hii ilitafsiriwa kama ujumbe kwa Mh. Edward Lowassa
Nashangaa Kikwete alipataje urais, uwezo wake ni mdogo sana ndio maana naombwa kila mara kuandamana naye kuokoa jahazi nchi za watu
Muda wa kuongea na wana Mtwara umepita. Serikali haiwezi tena kuongea nao. Gesi lazima itoke
Kelele za wana Mtwara ni sawa na kelele za chura.
Wapinzani ni wapuuzi, wanaongea bila ya takwimu
Watanzania hawana uwezo wa kuwekeza kwenye gesi. Watabaki kuwekeza kwenye matunda na juicetu
Kuanza mwakani, Tanzania itaanza kuuza umeme nchi za nje. Tutakuwa na umeme wa kutosha MW 7000