Upo zako mgahawani, utasikia kauli hizi zenye utata mtupu:
Mhudumu: Vipi
umeshawashughulikia wateja?"
Wateja: Aah! Sema kuhudumiwa, siyo kushughulikiwa.
Mhudumu: Karibu Masta, za
mzunguko?
Mteja 1 wa kiume: Mzunguko gani, acha ufala wewe.
Mteje 2: Oya shika hela yako (anatoa 10,000).
Mhudumu 2: Mzee hauna
ndogo? Tupe ndogo bhana, hii hatuna chenji.
Mteja 3: Oyyyyyyy naomba
kitumbua na maziwa. Jana
kitumbua chako kilikuwa kitamu kweli kweli.
Mhudumu: Weka kauli sawa, sio kitumbua changu, mi siyo mpishi.
Mteja 4: Ahaaaaaa, shee mkuuu ndugu yangu! Za
siku zako, unaendeleaje na hali?
Mhudumu: Wewe, kauli gani hizo, za siku zipi yani, dadavua?
Mteja: Oyy acha leo sina hela,
nitakupitishia.
Mhudumu: Weka kauli sawa, sema ntakupitia hela yako baadae, sio ntakuptishia!!Utanipitishia nini sasa, mti au? Acha ujinga.
KWENYE DALADALA
Konda: Makumbusho makumbusho,
vipi unaenda?
Abiria: Hamna siendi, ila
ukitaka nikupeleke nakupeleka chaap moja.
Konda: Naomba nauli mzee.
Abiria:
Ngoja ikisimama nakupa.
Konda: Acha ujinga weweeee!
Huku mtaani ukiambiwa kauli yeyote na vijana hawa, itafakari mara mbili kwanza!