PISTO LERO
JF-Expert Member
- Mar 8, 2011
- 2,819
- 1,458
Na nukuu.
Mwisho wa kunukuu.
Ndugu zangu watanzania haswa vijana ambao bado tungali na nguvu ya kupigania Haki na utu uliopotea katika Taifa hili. Kwa faida yetu kizazi chetu na wajukuu zetu, na tufanye hivyo sasa tusisubiri wajukuu zetu waje kucharaza viboko makaburi yetu. Tusisubiri hali iwe mbaya kama Congo ambapo vijana ambao ni nguvu kazi ya hilo badala ya kukaa kwao na kupigania nchi yao wao hukimbilia nchi za jirani na kusahau matatizo yaliyo wakimbiza nyumbani kwao na kuishia kujichubua na kunengua. Ni wakati wa kusema sasa basi na tuunganishe nguvuzetu kuliokoa taifa letu lisipotee.
Mwisho wa kunukuu.