Mdudu halisi
JF-Expert Member
- May 7, 2014
- 2,730
- 4,771
Juzi Jumamosi asubuhi nilikuwa naangalia kipindi cha watoto kwenye mojawapo ya vituo vya televisheni vya hapa nyumbani (Tanzani) Basi ukafika wakati wa 'Bungua Bongo', ndipo mtoto alipouliza swali kama ifuatavyo "Ni nchi gani ya Afrika ya Mashariki inaongozwa na Dikteta Uchwara?" Hilo swali lilinifanya nishikwe na bumbuazi na lililofuatiwa na kicheko kilichonifanya niondoke hapo sebuleni na hivyo sikuweza kufuatilia jibu lililotolewa lilitaja nchi gani.